''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, May 20, 2018

ROHO MTAKATIFU NA PENTEKOSTE

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Matendo 1:1-8, 2:1-6

Pentekoste ni siku ya 50 baada ya kupaa Yesu. Siku hiyo wanafunzi wake Yesu wakiwa pamoja wakisubiri ahadi ya Yesu, ukaja uvumi wa upepo wenye nguvu nao wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema kwa lugha nyingine. 

Yesu alijua ni jinsi gani Roho Mtakatifu alivyo wa muhimu sana na ndomana akawaambia wasiondoke Yerusalem mpaka wakatakapojazwa Nguvu ya Roho Mtakatifu. Unapookoka/ unapompokea Yesu unapata ile nguvu ya Roho Mtakatifu lakini unakuwa bado hujajaa, kwahiyo kunakuwa na hatua ya pili baada ya kuokoaka ambayo ndio kujazwa Roho Mtakatifu. Na alama mojawapo ya kwamba umejazwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, tunaona hata wanafunzi wa Yesu baada ya kujazwa wakaanza kusema kwa lugha nyingine.

Faida za Kujazwa Roho Mtakatifu
  1. Inakuwa nguvu zaidi ya kufanya kazi ya Mungu, inakupa nguvu katika huduma yako, Petro baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu akatangaza Neno la Mungu kwa bidii mpaka watu 3000 wakamkubali Yesu.
  2. Kunakusaidia kuomba kwendana na mapenzi ya Mungu, maana Roho ndani anakuwa anakusaidia kuomba
  3. Unapata uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na Mungu.
  4. Unakuwa unaweza kuomba kwa utulivu zaidi mbele za Mungu, ukiomba kwa kunena kwa lugha unakuwa huwezi kuwaza sehemu nyingine, sio kama ukiomba kawaida.
  5. Inakuwezesha kuimba kwa Roho
  6. Inakupa ufunuo ambavyo Mungu anataka uvifahamu
  7. Inakuwezesha kujenga imani yako zaidi 1Wakoritho 14:5



No comments:

Post a Comment