''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 24, 2018

TAMBUA MAJIRA/WAKATI WA KUACHWA (WAKATI WA KUBAKI PEKE YAKO)

Mhubiri: Mch. Nelson Kazimoto
Maandiko: Mathayo 27:45-46

Wewe kama mwanadamu ni vizuri ukatambua kuwa hapa duniani kuna nyakati nyingi za tofauti utakazopitia, na mojawapo ni wakati wa kuachwa. Kuna wakati Mungu ataruhusu ubaki peke yako kwa makusudi fulani, wakati wa kuachwa mwenyewe ili utimize kitu fulani au ili kusudi la Mungu litimie. Si mara zote unapopitia magumu ni kwasababu umetenda dhambi, bali Mungu ataruhusu upitie kwasababu ya lengo fulani.

Katika Biblia, Mungu ametufundisha hili, kuna watu waliopitia nyakati kama hizi na mmojawapo ni Yesu Kristo, katika Mathayo 27:46 "Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" tunaona Yesu aliachwa ili mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu litimie. 

Unapopita katika wakati huu kikubwa cha kufanya ni kutomuacha Mungu, hata kama utaona hakuna anayekujali, hakuna anayekusaidia, hata kama mateso yamekuwa makali sana, usimuache Mungu. Tambua kuwa Mungu yuko pamoja nawe, katika kila hitaji mshirikishe Yesu Kristo naye atafanya njia.

Mambo 3 ya Muhimu ya kufanya katika kipindi hicho ni:
   1. Ongeza sana IMANI yako kwa Mungu
   2. Ongeza sana UPENDO wako kwa Mungu
   3. Ongeza sana BIDII yako kwa Mungu, bidii ya kusoma NENO, KUTAFAKARI na KUOMBA

No comments:

Post a Comment