''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 2, 2018

WITO MKUU

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Andiko Kuu: Mathayo 28:18-20

Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi wake, mamlaka yote! yaani kila mamlaka ya mbinguni na dunia amepewa. Kwanini aliwaambia hilo kwa wakati ule, alikuwa anawahakikishia kwamba ndio muda wa kwenda kuhubiri sasa kwa nguvu zote. Yesu ndiye mwenye mamlaka yote mbinguni na duniani, na ametupa mamlaka hiyo tuitumie kuwafanya watu wengine wawe wanafunzi wake.

Kwasababu ya ile mamlaka juu ya kila falme, sasa tunaweza kutangaza habari zake kwa uhuru na kuharibu kila pando la shetani katika watu na kuwafanya wawe wanafunzi wa Yesu. Mamlaka yenye nguvu ndio inayotawala.

Wito wetu mkuu ni kuwafanya watu waje kwa Yesu. Kuwaambia watu habari njema za Yesu, na wakisha wakimkubali kuwalea na kuwafundisha ile wawe wanafunzi wa Yesu.

'Kwenda' inamaanisha kutoka mahali ulipo na kwenda kuwawahubiri wengine kuhusu ile mamlaka uliyopewa. Unajua unaweza ukawa na nguvu ya kufanya kitu lakini ukawa huna mamlaka ya kukifanya hicho kitu, kwa ngazi uliyonayo huruhusiwi kufanya kicho kitu. Polisi wa barabarani akinyosha mkono tu gari linasimama na kwasababu tu ya ile mamlaka aliyonayo, na kwa upande mwingine polisi mwenye mamlaka tayari asipo yatumia mamlaka yale au asipotambua kuwa yeye ana mamlaka, hataweza kusimamisha magari. Sasa sisi tumepewa ruhusa ya kutumia mamlaka ya Yesu, alitupa kazi ya kufanya ya kuwaleta watu kwa Yesu, lakini akatupa na mamlaka ya kutuwezesha kutimiliza kazi hiyo.

Mamlaka ya Yesu umepewa, sasa nenda nje ukaitumie ile mamlaka uliyopewa kuwaleta watu kwa Yesu. Kila Mkristo, umeitwa kufanya kazi hii, ya kuwaleta watu kwa Yesu. Itende kazi hiyo kwa bidii kwani kila mtu kazi yake itakaguliwa.

No comments:

Post a Comment