''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 28, 2018

KANISA KUADHIMISHA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Vicent Samwel Malenda
Maandiko: Matendo 1:8, 2:1-4

Nguvu ya Roho Mtakatifu, nguvu ambayo Yesu Kristo aliiahidi mwenyewe wakati anaondoka, kwahiyo leo tunamkumbusha nguvu Yesu aliyotuahidi kwamba itakuja kwetu.

 Matendo 1:8 "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

Nguvu hii ni ahadi na ni kwa ajili yako, ukiwa na kiu ya kuipata nguvu hii itakuja kwako, Roho Mtakatifu ataingia na kujaa ndani mwako. Bila nguvu hii haiwezekani kuishi maisha matakatifu, nguvu hii ndio inayoweza kukusaidia usitende dhambi. Roho Mtakatifu anapokuja ndani mwako anabadilisha maisha yako, haiwezekani nguvu hii ikashuka ndani mwako alafu ukabaki vilevile.

Matendo 2:1 "Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."

Namna ya kutunza /kuiendeleza nguvu hii ndani mwako
1. Ishi maisha matakatifu, Roho Mtakatifu ni mtakatifu sana kwahiyo ukijichafua tu ndani mwako Roho Mtakatifu  anaondoka. 
2. Lazima umtangaze Yesu Kristo, upeleke injili, lazima uwaambie watu wengine kuhusu Yesu Kristo. 

No comments:

Post a Comment