''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 21, 2018

KUUFANYA IMARA WITO/WOKOVU WAKO

Mhubiri: Dk. Emmaculate Migula
Maandiko: 2Petro 1:2-11, 3:1-7

Petro aliandika hii wakristo kwasababu aliona kuna mafundsho ya uongo yameingia kwenye miji yao, yanayosema kwamba Yesu aliyeahidi kurudi hatarudi tena kwasababu amekawia sana; na ndomana pia 2Petro 3:1-7 anawakumbusha tena kuhusu kitu hicho hicho kwamba wasisikie huo uongo. 

Neema ya Mungu imetuletea wokovu na pia imetuwezesha kuishi maisha ya utauwa/matakatifu, ndio ni kweli umeokolewa kwa neema lakini Lazima maisha yako yathibitishe kuwa kweli umeokolewa.

NI kweli umeokolewa lakini jinsi gani ya kumsubiri Yesu mpaka arudi kunahitaji bidii yako ya kuendelea kujitunza kila siku katika safari yako. Ndio umepewa neema ya wokovu lakini wewe ndio wa kujitahidi kuwa karibu na Yesu ili uendelee kuwa mtakatifu. Kuna watu wanasema ukioka tu kwasababu ya ile neema ile iliyokuokoa basi ukifanya lolote utaenda tu mbinguni, hapana huo ni uongo, ni lazima uishi maisha matakatifu.

Ni kweli Mungu katupa kila kitu cha kuwa mtakatifu, ndio tumeamini lakini kuna vitu vya kuvifanyia kazi sisi ili kuweka imani yetu katika matendo. Baada ya kuokoka ni lazima uzae matunda. Kwanzia mstari wa 5-7 Petro ameeleza vitu vya kuongeza baada ya kuokoka

2Petro 1:5-7 "Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo."

Ndani ya wokovu wako lazima uwe na Wema, Maarifa, lazima uwe na Kiasi, lazima uwe na saburi/subira ambapo ndani mwake kuna uvumilivu, na vya mwisho lazima uwe na Utauwa/utakatifu na Upendo. Wokovu ni zaidi ya kuitwa mlokole, wokovu ni maisha.

No comments:

Post a Comment