''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 14, 2018

MKRISTO IMARA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Waefeso 6:10-20

Wakati ule mtume Paulo alikuwa kwenye inchi yenye utawala wa Rumi, kwahiyo akatoa mfano wa kama askari wa kirumi walivyokuwa wanavaa silaha zote tayari kwa lolote. Mkristo imara ni yule tu anayevaa silaha zote, sio baadhi ya silaha hapana bali unapaswa kuvaa silaha zote ili uweze kushinda hila za shetani, kwa maneno mengine kumbe huwezi kushinda hila za shetani bila kuvaa silaha zote. 

Pia ili uwe Mkristo imara ni lazima uwe na uhusiano mzuri na Mungu. Uhusiano huo unaimarishwa kwa Kusoma Neno la Mungu kwa bidii na kuwa mtu wa maombi. Je utawezaje kumshinda shetani kama husomi Neno la Mungu na wala huombi? huwezi kumshinda shetani kwa nguvu za kimwili za misuli, kama huna nguvu za kiMungu shetani atakuchezea ovyo-ovyo lakini kama ukiamua kuwa na nguvu za kiMungu shetani atakukimbia.

Katika siku yako kuna masaa 24, je umetenga masaa mangapi kwa ajili ya Mungu? kwa ajili ya kusoma Neno la Mungu na kuomba? au masaa yote unatumia wewe mwenyewe na ratiba zako? Tenga muda kwa ajili ya Mungu wako nawe utaimarika zaidi kiroho.

Simama imara, usiruhusu mambo ya dunia yakusogeze, ni kweli hapa duniani kuna mambo mengi lakini ni lazima ujihakikishe kuwa hayo yote hayakusogezi hayakufanyi uache kuwa mtakatifu, NI LAZIMA UWE MTAKATIFU

1Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana."

1Petro 1:16 "kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."  

No comments:

Post a Comment