''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 7, 2018

JIFUNZE KUMSIKILIZA MUNGU

Mhubiri: Mr. Victor Adrian
Neno: Mwanzo 22:1-12

Je, wewe ni mtu ambaye unaomba tu lakini hutaki kumsikia Mungu?, Kupeleka maombi yako kwa Mungu sio kitu kibaya lakini unatakiwa umupe Mungu muda wa kuongea na wewe. Tunatakiwa tumsikie Yeye, Mungu anataka sana tumsikilize yeye, ifike mahali uwe na mawasiliano mazuri na Mungu. Mawasiliano yana pande mbili; wewe kusema na Mungu kukwambia. 

Kumsikiliza Mungu kwa umakini si rahisi sana, inabidi ujizoesha kila siku mara kwa mara upate muda na Mungu wako. Ili umsikie Mungu ni lazima uwe na mawasiliano nae mazuri, uhusiano baina yenu uwe mzuri. Na sio mara zote Mungu atakawambia kile unachotaka ukisikie lakini atakwambia kile anachoona ni sahihi kwako, unachotakiwa ni kutii.

Mungu alimwambia Ibrahimu akamtoe sadaka mwanae pekee tena aliyemsubiri kwa muda mrefu sana, lakini Ibrahimu hakujiuliza sana bali akatii, ilikuwa si kitu rahisi lakini Ibrahimu alitii. Mungu anaangalia utayari wako wa kufanya kile alichokuelekeza. 

No comments:

Post a Comment