''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 30, 2018

JITAKASE UWE CHOMBO CHENYE HESHIMA KWA AJILI YA KRISTO

Mhubiri: Mzee Kiongozi, Dr. Mumghamba
Maandiko: 2Timotheo 2:20-25, Mathayo 7:21-23, 13:8-9

Nyumbani kwako una vyombo vya aina nyingi, vyenye heshima na visivyo na heshima,  na mgeni wa heshima akikutembelea nyumbani kwako hutampa chai kwenye kikombe cha plastic bali kikombe cha udongo kwasababu ya thamani yake. Vivyo hivyo sisi ni vyombo vya Mungu jinsi unavyojisafisha na kuishi maisha matakatifu ndivyo Mungu atakavyozidi kukutumia zaidi na zaidi. Mungu anaangalia ndani ya moyo. 

Efeso 4:21-24 "21 ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, 22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; 23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; 24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli."

Ili uwe chombo kisafi ni lazima uwe tayari kuacha vitu ambavyo vinakurudisha nyuma na kuwa tayari kuishi maisha matakatifu.

Warumi 13:11-14 mtu huwa haendi mjini na nguo ya kulalia bali huwa anaivua na kuvaa nzuri, vivyo hivyo ni lazima tubadilike, ili Yesu akutumie ni lazima ubadili mambo unayofanya. 

Ili uwe na maisha matakatifu ni lazima tabia hii ya kuchagua nini cha kufanya na nini cha kuacha iwe tabia ya kila siku, hili ni zoezi la kila siku, na uwe makini usizidiwe na muda maana kama Yesu akija ukakutwa bado hujaacha kitu ambacho ulitakiwa kuacha basi Yesu atakuacha hatakwenda na wewe. Je uko tayari kuacha matendo mabaya?

No comments:

Post a Comment