''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, September 23, 2018

HATARI YA KUKOSA UAMINIFU MBELE ZA BWANA

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Neno: 2Wafalme 5:15-27 

Gehazi mtumishi wa Elisha, hakuwa mwaminifu kwa bwana wake, alimdanganya Elisha, akadhani kuwa bwana wake hatagundua. Uaminifu mbele za Mungu ni kitu muhimu sana. Wakati wa sasa kuna nafasi nyingi za kupata fedha kwa njia isiyo sahihi, lakini wewe kama mtu ulieyeokoka hupaswi kuwa na tamaa. Hupaswi kutumia njia za magendo kupata hela au kitu unachohitaji, bali subiri kwa uaminifu mbele za Bwana naye hatakuacha. 

Kushindwa kuishi kwa uaminifu mbele za Bwana huwa kunaleta madhara. Gehazi aliposhindwa kuwa mwaminifu kulimpelekea kupata ukoma wa Naamani. Wewe binafsi ndiye unayejua maisha yako, ndiye unayejua kama ni mwaminifu mbele za Mungu au lah. 

Ni wakati sasa wa kutubu, kumwambia Yesu umekosa kwa kutokuwa mwaminifu kanisani, kazini, kwenye biashara zako. Jisalimishe mwenyewe kwa Yesu ili aweze kukusamehe. 

No comments:

Post a Comment