''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, September 17, 2018

UFALME WA KI-MUNGU MAISHANI MWETU

Mhubiri: Mrs. Masembo
Neno: Mathayo 6:7-10, Luka 11:1-2

Hapa duniani kuna falme nyingi, lakini falme hizo zote si sawa na Ufalme wa Mungu, Ufalme wa Mungu ni wa tofauti sana. Ufalme wa Mungu unamaanisha uongozi mkuu wa kiroho. Hapa Yesu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake jinsi ya kuomba, sala hii aliowafundisha ilikuwa ya tofauti. Ndio watu huwa wanaomba lakini wakiomba huwa wanalenga nini?, nini ni kusudi lao?, mafarisayo walikuwa wakiomba wanaomba mbele za watu ili wapate sifa, sasa sisi hatutakiwi kuwa hivyo; bali tuombe kwa lengo la Yesu kutusikia.

Katika sala ile Yesu aligusia mambo mengi, mojawapo ni hili la Ufalme wa Mbinguni uje kwenye maisha yako. Inamaanisha ule ukuu wa Mungu uje maishani mwako, ni kitu kikubwa sana kinakuja kwako. 

Jinsi Kutunza Ufalme wa Mungu Katika Maisha Yako
1. Uishi maisha Matakatifu, ili Roho wa Mungu aendelee kukaa ndani mwako ni lazima uishi maisha ya utakatifu
2. Lazima ujikane mwenyewe,  Luka9:23 "Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate".
3. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na nidhamu binafsi katika ratiba yako ya kusoma Neno la Mungu na kuomba, pia katika maisha yako kwa ujumla umuwakilishe Yesu vizuri mbele za watu.
4. Lazima uamue kuwa mtu wa rohoni na kukua kiroho, Heb 5:11-14 unataka kukua ni lazima uwe unasoma sana Biblia, ukikua shetani hatakuchezea utajua jinsi ya kutambua hili linatoka kwa Mungu au kwa shetani. Penda kukua kiroho usiwe mtoto kila wakati katika mambo ya kiroho, usiwe mtu wa maziwa tu anza kula chakula kigumu. Kila siku uwe tayari kujifunza kutoka kwenye neno la Mungu usilizoee Neno bali kila siku uwe tayari kujifunza kitu kipya.

No comments:

Post a Comment