''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, November 11, 2018

KUISHI KWENDANA NA NENO LA MUNGU

Mhubiri: Mzee wa Kanisa, Leandri Kinabo
Maandiko: Yakobo 1:19-27, Mhubiri 9:17, Warumi 1:16, Mathayo 7:21-23

Yak 1:19-27 "Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 20 kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. 22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. 26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. 27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa."

Sisi kama watu waliookoka inapaswa kuishi kwendana na maagizo ya Mungu. Biblia imeweka wazi kabisa kuwa makini na jinsi unavyoishi, kuna wengine watasema Bwana Bwana tulifanya kazi zako lakini Yesu atasema hawajui kwasababu hawakuishi kwendana na Neno la Mungu, hawakuishi maisha ya utakatifu. Wokovu ni zaidi ya kusema kwamba umeokoka, wokovu ni maisha yako ya kila siku na Yesu.

No comments:

Post a Comment