''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 18, 2018

MAISHA KATIKA NENO LA MUNGU

Mhubiri: Mch. Kiongozi, Abdiel M. Mhini
Maandiko: Yohana 1:1-5, Isaya 55:10-11

Neno la Mungu ndilo unalohitaji katika maisha yako ya kiroho, ndilo unalohitaji katika maisha ya ushindi na mafanikio. Bila Neno la Mungu hutaweza kupata mafanikio ya kweli.

Yohana 1:1-5 "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza."

Uumbaji wote ulitoka kwenye Neno, naye Neno alikuwa Mungu. Neno la Mungu ni mwanga maishani mwako,  Neno la Mungu ni nuru ambayo hakuna giza linayoishinda. Kwahiyo Neno la Mungu ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako. Weka bidii ya kusoma Neno kila siku utaona maisha yako yaanza kubadilika.

No comments:

Post a Comment