''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, November 26, 2018

UTOSHELEVU WA MWANADAMU

Mhubiri: Mzee wa Kanisa, Godfrey Zayumba
Maandiko: Mhubiri 1-2

Hichi kitabu kiliandikwa na Mfalme Suleimani, hapa anatoa hitimisho ya mambo yote aliyoyaona huku duniani. Mfalme Suleiman alikuwa ni mfalme tajiri sana kwahiyo aliamua kujaribu kila kitu kinachowezekana vyote vya Ki-Mungu na visivyo vya Ki-Mungu.

Pia alikuwa ni mtu mwenye hekima sana kwahiyo hapa anahitimisha kuwa hakuna kipya chini ya jua, mambo yote ni ubatili, ubatili mtupu. Mungu anachohitaji kwetu ni tumpende Yeye na tumshukuru na kutosheka na vile anavyotupatia. Sisi wanadamu tunatafuta pesa mchana na usiku lakini haturidhiki bali kwake Mungu pekee tunatoshelezwa. Mungu anataka uwe na unyenyekevu mbele zake.

 "16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; 17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. 18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. 19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. 20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? 21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu." Luka 12:16-21

Mungu anataka urudi unyenyekee, hata kama Mungu amekubariki kwa vingi usijikweze, bali umtukuze Yeye aliyekupa. Usizani kuwa ulifanikiwa kwasababu unajua sana bali utambue kwamba ni neema Mungu iliyokuwezesha. Mungu anataka uone kuwa mali hizi ni sifuri bali Yeye ndio wa muhimu. 

No comments:

Post a Comment