''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, December 10, 2018

MAMBO YANAYOLETA UHAI KATIKA MAISHA YAKO YA KIKRISTO

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Kutoka 20:1-6, Warumi 2:13

Wewe kama mwanadamu unahitaji maisha yaliyo hai, uhai wa maisha ya kikristo lazima ujikite kwenye Neno la Mungu, kwa maana nyingine bila kusoma Neno la Mungu huwezi kuwa hai kiroho. Watu wengi sasa wanapenda sana injili ya mafanikio, ya kwamba utapata hichi utapata kile, lakini je injili ya maana ni ipi?, chanzo cha kweli ni nini?. Ili kujua injili na kuwa hai ndani mwako ni lazima uwe unasoma Biblia, mahitaji ya kibinadamu yapo, ndio unahitaji kuendelea, lakini kama kweli unataka kuendelea ni lazima uache na Neno la Mungu kwanza. Neno la Mungu ndio msingi wetu, kuna nguvu kubwa sana ndani ya Neno la Mungu. Kama unataka mafanikio ya kweli soma sana Biblia kuwa na uhusiano mzuri na Yesu pia fanya kazi kwa bidii.

Dondoo za Muhimu:

1. Wenye haki sio wale wanaosikia Neno la Mungu tu bali ni wale wanaolitii, ni wale wanaolitenda. 
Warumi 2:13 "Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki."

Kila siku tenga muda wa kusoma Neno la Mungu, soma hata sura kadhaa, siku isipite bila kusoma Neno la Mungu. Hata siku moja hakuna nguvu za kiroho bila Neno la Mungu.

2. Shika sana maagizo aliyotuachia Yesu, ukisoma Mathayo 5-7 anaelekeza mambo mengi sana, jinsi tunavyotakiwa tuishi maisha ya Kikristo. Mathayo 8:31-32, ukiifahamu kweli na hiyo kweli itakuweka huru, Kweli ni Neno la Mungu.

3. Mtangaze Yesu, Yesu alituachia agizo kuu la kwenda kuwafanya wengine kuwa wanafunzi wake, Nenda mtaani, hospitalini kawashuhudia kuhusu Yesu.

4. Maisha ya Kikristo lazima yawe na Maombi, ni lazima uwe unaomba, maombi yanatakiwa yawe ni maisha ya kila siku, Warumi 8:26-27 Roho wa Mungu anatusaidia udhahifu wetu.

5. Lazima uvae silaha zote ili kuwa tayari kumshinda shetani katika ulimwengu wa roho, kwa maana vita vyetu si katika ulimwengu wa nyama bali wa roho; Waefeso 6:10-11.

No comments:

Post a Comment