''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 16, 2018

MAISHA YA KUMTEGEMEA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Maandiko: Warumi 8:26-27

Sio kila Mkristo ni Mpentekoste bali kila Mpentekoste ni Mkristo. Pentekoste ilikuja baada ya Roho Mtakatifu kuja duniani. Kazi kuu ya Roho Mtakatifu ni kuliandaa kanisa, kukuandaa wewe kwa ajili ya kumpokea Bwana Yesu atakaporudi kwa mara ya pili.  

Mojawapo ya madhara ya dhambi ni kujisikia kuwa umekamilika ndani mwako bila kumuhitaji Mungu, ukijihisi tu hupendi kumtegemea Mungu ujue dhambi imekutafuna, imekufanya ujisikie hivyo. 

Ni lazima ujifunze kumtegemea Roho Mtakatifu maana Yeye ana faida nyingi sana kwa ajili yako. Mtegemee Roho Mtakatifu kwa asilimia zote utaona maisha yako yakibadilika. 

Warumi 8:26-27 "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu."

Wewe binafsi huwezi kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu, lakini ukimtumia Roho Mtakatifu ambaye anajua siri za Mungu utafanikiwa katika kuomba yulee. Muda mwingine tunaomba lakini hatujibiwi kwasababu hatuombi kwendana na mapenzi ya Mungu.

Mungu anataka kukujibu kabisa maombi yako lakini kama hauko imara katika ufahamu wako kanuni zake, kwasababu Mungu anataka tuomba vizuri(right) lakini pia vitu vyenye maana (make sense), sasa haya yote hutaweza bila kumtegemea Roho Mtakatifu.

Dakika moja kuomba ukiwa katika Roho Mtakatifu ina faida kubwa sana kuliko maombi ya lisaa limoja bila Roho Mtakatifu.

- 1Wakortho 2:15-16, vitu vyote, mashauri yote tunayohitaji binadamu yamewekwa ndani ya Roho Mtakatifu, kwahiyo kama utaanzisha uhusiano imara na Roho Mtakatifu utapata faida sana.
- Yuda 1:20, sasa ili kufanikiwa inabidi kwanza kujijenga, kujishikiza kikweli kweli ndani ya Roho Mtakatifu kumtegemea kikweli kweli Roho Mtakatifu, kutengeneza tabia ya kuwa tegemezi kwa Roho Mtakatifu.

No comments:

Post a Comment