''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, August 25, 2019

RUDI MSALABANI

Mhubiri: Mch. Prof. Matto
Maandiko: 1Wakorintho 1:18-31

Paulo alikuwa analionya kanisa la Korintho, kwasababu lilianza vizuri sana katika wokovu lakini badae likapoa na kuanza kuruhusu mambo ya kidunia kuingia kanisani. Mji wa Korintho ulikuwa ni wa kibiashara na wenye mchanganyiko mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali kwahiyo hata maovu yalikuwepo sana. Sasa zile roho chafu za ule mji zikaanza kuingia katika kanisa, matatizo yakaanza. Kitu hicho hicho ndicho kinachotokea sasahivi kwenye makanisa yetu, roho chafu za dunia zimeaza kuingia makanisani, watu hawaishi tena kama watu waliokoka bali kama watu wa mataifa wasiookoka; ndio maana ujumbe wa leo unakwambia 'Rudi Msalabani'. 

Mambo mengi yamekuwa hayaendi kama ulivyotarajia kwasababu umemuacha Mungu wa kweli na kuanza kuzitumainia akili zako, Yesu Kristo anakwambia 'Rudi Msalabani', tafuta kutengeneza na Mungu wako binafsi. Kumbuka Mungu alikokutoa uko hivyo ulivyo kwasababu Mungu amekusaidia. Neema sasa bado ipo tengeneza maisha yako na Yesu.

Yesu Kristo alikuja kutukombia wanadamu kwasababu ya upendo wake mkuu, Yesu Kristo ni halisi ni wa kweli katika maisha yako, hatuishi kwasababu ya nguvu ya mwanadamu bali tunaishi kwasababu ya Neema ya Mungu, kwahiyo usimsahau Mungu, patana na Yesu Kristo leo!

Unajua kwa watu wasiomjua Yesu Kristo, habari za msalaba ni bure kwako hawaoni uthamani wowote, kwasababu wanatumia hekima ya kibinadamu wengine wanauliza huyo Yesu yuko wapi wanataka kumuona katika ulimwengu wa mwili. Lakini kwako unayemjua Yesu mshike sana maana umepata neema, basi tengeneza mambo yako na Yesu. Kumbuka kazi kubwa sana aliyeifanya Yesu Kristo pale msalabani kwa ajili yako na mimi.

shetani anaweza kuwa anaongea ndani mwako anakwambia wewe si kitu, mjibu kwamba wewe ni kitu cha thamani sana kwasababu wewe ni mtoto wa Mungu, Pale msalabani Yesu Kristo alilipa gharama ya ukombozi wako, ni wewe kuamua tu leo kugeuka na kumrudia Yesu Kristo ili ayaongoze maisha yako kwasababu wewe mwenyewe hutaweza kuishi maisha matakatifu bila Yesu. Rudi kwa Yesu sasa

No comments:

Post a Comment