''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 9, 2014

UMOJA NA NGUVU ILIYO NDANI YA UMOJA

MHUBIRI: Mr.Fabian Masembo
Maandiko: Zaburi 133:1-3

Watu wakae pamoja lakini sio kukaa tu pamoja bali kwa umoja. Mfalme alifananisha kama mafuta au umande kwasababu ukiangalia mafuta yanavyo tiririka huwa hayaachani pia hata umande hauachani huwa unatiririka pamoja. 

Mwanzo 1:26, Mungu alisema tufanye mtu kwa mfano wetu angeweza kusema kwamba tufanye mtu kwa mfano wangu lakini hakusema hivyo, kumbe umoja huu umeanzia Mbinguni, Mwanzo 2:18, hapa pia Mungu aliona sio vema mtu akae pekee yake Mungu anapenda tuwe na umoja, angeweza kumfanya mtu awe pekee yake na kuishi pekee yake lakini hakufanya hivyo, Yohana 17:11, Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo, kumbe kule mbinguni palishakuwa na umoja na anataka na sisi tuwe na umoja, Yesu aliona wanafunzi wake walivyokuwa hawana umoja kati yao.  Yohana 17:20-23, 

Kwanini tuishi pamoja? au Kwanini tuwe na umoja? kwanini tuishi pamoja kwa umoja? sababu ya kufanya hivyo ni
 1.Tunahitaji kusaidiana wakati wa majaribu,upweke na uhitaji, soma Mhubiri 4:9-12 na Warumi 15:14, sasa kama ukiwa pekee yako nani atakuonya kama ukifanya makosa. Unaweza ukawa huendi vizuri lakini kwasababu uko mwenyewe huwezi jua matendo yako kama ni mabaya. Pia unahitaji/tunahija umoja ili usaidiwe/tusaidiane, unapokuwa umekata tamaa utapata mtu wa kukutia moyo. Wagalatia 6:1 inaelezea kwamba nyie mlio wa roho mrejezeni sasa kama uko mwenyewe nani atakurejesha? 

2. Tunahitaji umoja ili kutimiza kazi ya Mungu, Mathayo 18:19-20 "19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao." kwahiyo unaona umuhimu wa kukaa pamoja pia katika Matendo 4:23-31 na Matendo 12:5 Kanisa liliomba kwa bidii kwa ajili ya petro sasa kama petro angekuwa pekee yake angeombewa na nani?, hawa watu walikuwa na umoja ndomana petro alivyowekwa gerezani kanisa huku nyuma likaanza kuomba. Kanisa la Mungu ni kama mwili vinafanya kazi kwa pamoja kwahiyo Mungu hivi leo anakukumbusha Wewe/mimi kwamba tunatakiwa kukaa PAMOJA na kwa UMOJA, kama ni kwenye injili tunashiriki wote wengine wanatoa hela wengine wanaenda kuhubiri mikoani, wengine wanabaki kuomba, ukitaka kuona kazi ya Mungu ni rahisi na upate baraka tufanye kwa pamoja na umoja. 

3. Tunahitajiana kwasababu inakuwa kama ulinzi kwetu soma Mhubiri 4:12, Kumbukumbu la torati 32:30 "Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?" iko nguvu katika umoja sio kwamba umeletwa tu hapa duniani ili uishi kama unavyotaka lakini ili uishi kwa umoja.

Ili umoja uwepo ni lazima vitu vifwatavyo viwepo
1.AMANI
2.UPENDO
3.LUGHA MOJA
4.USEMI MMOJA

Kunawezekana kukawa na lugha moja kati yetu yaani kama kiswahili  wengi wataelewa lakini kusiwe na usemi mmoja. Kuwa na lugha moja sio shida lakini kuwa na useme mmoja ndipo kuna tatizo, tunaweza kukubaliana kufanya kitu fulani ikatumika kiswahili ambacho kinaeleweka lakini watu wasifanye kile kitu, Mwanzo 11:1-4 walikuwa na lugha moja lakini pia walikuwa na usemi umoja yaani wakikubaliana kufanya kitu wanafanya vile vile walivyokubaliana, lugha waliielewa lakini kulikuwa na kitu za ziada kuwa na usemi  mmoja kwasababu ya usemi mmoja baada ya kuambiwa tufanye matofali wakaanza kufanya matofali. 

Lakini katika umoja shetani anaweza kuleta majaribu ili umoja wenu uondoke, lakini kama kweli mmejifunza kukaa pamoja kwa umoja na Roho wa Mungu akiwa ndani yenu hamtagombana mfano Mwanzo 13:1-5, Abrahamu na lutu walivyokuwa wanakaa pamoja baada ya kila mmoja kubarikiwa kwa wanyama majaribu yalipotokea wachungi wao waligombana lakini wao hawakugombana walisuluhisha kwa amani na kugawana maeneo kwa upendo. Mfano mwingine ruth na mkwe wake, david na jonathani, pia kanisa la mwanzo Matendo 2:42-47, Efeso 4:1-6



Mr Fabian Masembo, kushoto akiwa anahubiri na mtafsiri wake(Mr.Okech)

No comments:

Post a Comment