''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 30, 2019

FAIDA 10 ZA MAOMBI, KATIKA MAISHA YA KIROHO

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Maandiko: Wakolasai 1:9-11, 4:3-4

Maombi ni silaha kubwa sana katika maisha ya kiroho, mkristo ambay e hasomi Neno la Mungu wala haombi hawezi kufanikiwa kuishi maisha matakatifu. Na Msingi wa kuomba ni huu, hatutakiwi kuomba ili upate kitu bali fanya maombi kama mawasiliano yako na Mungu wako. Maombi ni mawasiliano kati yako na Mungu. Tumeitwa au tumeumbwa ili tuishi maisha matakatifu.

Faida za Kuomba Kila Siku

1. Maombi yanakusaidia kujua mapenzi ya Mungu.
2. Maombi yanakuwezesha kuishi maisha matakatifu  Wakolosai 1:10
3. Maombi yatakusaidia kumpendeza Mungu.
4. Maombi yakuwezesha kuzaa matunda ya Roho; sana sana pale unapoomba kwa kunena.
5. Maombi yakusaidia kumjua Mungu zaidi.
6. Maombi yanakupa Nguvu za Kiroho, Efeso 4.
7. Bring great endurance and patience romans 8:6.
8. Maombi yanakupa moyo wa shukrani mbele za Mungu.
9. Maombi yanafungua milango iliyofungwa na kukupa fursa mpya.
10. Maombi yanatoa Ufunuo wa Kweli na Nguvu ya kuongea Kweli, Wakolosai 4:4.

No comments:

Post a Comment