MHUBIRI: Mch. Kiongozi Mhini
Maandiko: Marko 16:15-18
Umisheni ndiyo moyo wa Mungu ndio kusudi kubwa la Mungu,
kusudi maalumu ni kumuokoa mwanadamu, Na alilonena akiwa dunia alikuwa ananena
kile alichopewa na Baba yake kuzungumza, Marko 16:15-18, haya ni maneno ya
mwisho aliyowaachia wanafunzi wake wakati anakaribia kurudi Mbinguni, maeno haya ni ya msingi sana, ndio
yanayokamilisha ujio wake wa kuja duniani. Hakuna anayeokolewa na kukaa tu ni
lazima uwe na shughuli maalumu. Sisi kama watu tuliookolewa na Yesu tunawajibu ufwatao:
1.KUMUWAKILISHA BWANA YESU HAPA DUNIA, Matendo 1:8, kumuwakilisha Jina lake maeneo ambayo hayajafikiwa
2.KUWAFANYA
WALIOOKOLEWA KUWA WANAFUNZI, yani waliookolewa kuwafundisha Neno la Mungu ili na
wao wachukue jukumu lilelile la kuwashuhudia wengine habari za Yesu
3.KUWAJULISHA NGUVU YA UTENDAJI AMBAYO
NDIO ROHO MATAKATIFU, Roho Mtakatifu ni nyenzo ya kupeleka injili
4.KUWA
MCHUNGAJI MWEMA, chunga uchungaji wako na wapeleka kondoo katika
malisho mema
5. KUWAPELEKA WATENDA KAZI SHAMBANI, Warumi 10:15
Ni jukumu letu
kupeleka injili mahali mbalimbali yasiyofikiwa kwa kuchangia na kuwaombea Watu wali tayari kwenda maeneo hayo. Changizo kwa ajili ya umisheni hazijaanza leo Wafili
4:14-20, watahubirije wasipo pelekwa, swala la kuwapeleka halikuanza leo ni
kanuni kabisa ambayo ipo kwenye biblia, Yeremia 47:7, hatuta kwenda wote lakini
tutaenda kwa changizo zetu, Bwana Yesu anapenda kumuona mtu anayetoa kwa moyo
wa ukunjufu na kwa moyo wa kupenda, wamishenari ni wajumbe, ni wawakilishi wa
jina la Yesu hebu tuwabeleke wamishenari, na Bwana Yesu atajitokeza katika
maisha yako hautapungukiwa tena.
Amina
ReplyDelete