''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, September 4, 2016

SIRI YA UNYENYEKEVU

Unyenyekevu ni Nini?
Tafsiri 4 za Unyenyekevu:
1. Unyenyekevu ni hali ya mtu kujishusha licha ya hadhi, haki au kiwango alicho nacho.
2. Unyenyekevu ni hali ya mtu kuonyesha heshima na kujali kwake kwa watu wengine bila kujali ukubwa wala udogo wa kiwango kiwango chao chao cha maisha nk.
3. Unyeyekevu ni hali ya kuudhibiti moyo wako usitawaliwe na kiburi, jeuri, mavivuno wala dharau kwa mtu wa aina yeyote.
4.Unyeyekevu ni hali ya kuinua kiwango cha thamani ya watu wengine na kuwaleta katika kiwango chako na kuwa ona kuwa wao pia wana thamani kubwa kama wewe ulivyo.
 
SABABU 5 ZA KUNYENYEKEA
Why Humility is Important?
1. Tunapaswa kuwa wanyenyekevu kwasababu hatujui kesho yetu.
    Yakobo 4:13-15 "13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. 15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi."
    
2. Tunapaswa Kunyenyekea kwasababu Kiburi Kinaleta Madhara Makubwa na Unyenyekevu Unaleta Baraka.
Mithali 18:12 "12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu."

3. Tunapaswa Kuwa Wanyenyekevu kwasababu Mungu Huwapinga Wasio na Unyenyekevu na Huwapa Neema Wanyenyekevu.
Yakobo 4:6 "6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu."

4. Tunapaswa Kunyenyekea kwasababu Hatujui sana Kuhusu Madhaifu Yetu na Tunahitaji Watu Wengine watusaidie kwa Upendo. (We are limited in our self-knowledge).
Zaburi 141:5 "5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao."

5. Tunapaswa kuwa na unyenyekevu kwasababu bila ya Unyenyekevu hatutauona ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18:3-4 "3. akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni."
 
 
 

9 comments:

  1. Powerful massage God bless you

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kwa kutoa somo zuri sana kwa wana wana wa ulimwengu

    ReplyDelete
  3. Ndicho ninachotafuta kumjua vizuri Mungu. Nimebarikiwa sana endelea kutupa Neno la uzima tupone

    ReplyDelete
  4. May God bless you. Asante sana kwa neno ili

    ReplyDelete
  5. Thank you for a good lesson God bless you

    ReplyDelete
  6. Thanks and I have a swell give: Where To Remodel House house repair near me

    ReplyDelete
  7. thanks i am very understanding, god bless you

    ReplyDelete