''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, August 28, 2016

JIHADHARI NA MAADUI WA NDANI

Mhubiri: Mchungaji Sanga
Maandiko: Matendo 20:17,28-31,
 
Adui wa ndani ni mbaya kuliko wa nje kwasababu ni vigumu kumtambua, Paulo aliambia kanisa la wakati ule kwamba miongoni mwao watainuka watu watakao haribu lile kundi. Na ndio shida ya kanisa la leo linakaribiwa na adui wa ndani, na adui wa ndani ndio anayesababisha upotovu anapotosha kanisa kutoka kwenye ile kweli watu wanabaki wanachanganyikiwa wanakosa mwelekeo wanashindwa kujua wasimamie wapi kwasababu wameshambiliwa na adui wa ndani wameshambuliwa kimapokeo wameshambuliwa kimafundisho, wengine wamenyweshwa chumvi na mambo mengine ya ajabu.
 
    Kanisa la kwanza adui alishambulia kwa nje, watu waliomuamini Yesu walikatwa vichwa  bila kumuacha Bwana lakini nyakati za leo mashambulizi yako ndani. Vita au adui wa ndani analeta uharibifu mkubwa  tena kwa siri ndani ya waaminiyo.
 
KAZI YA ADUI WA NDANI AKIINGIA KWAKO
  1. Anaharibu maono yako, anavuruga mikakati yako  
  2. Anadhohofisha kazi ya Mungu, anafanya watu wasiwe na hamu ya kujitoa
  3. Anagawa kundi anasababisha matengano, kanisa linakuwa limejigawa vipande vipande hataki watu wamuite Mungu kwa pamoja kwa sauti ya umoja, baba ana mipango yake mama ana mipango yake na watoto wana mipango yao wakati hiyo ni familia moja, hawa wa Apolo hawa wa Paulo, analeta mitazamo tofauti.
  4. Anakatisha tamaa watenda kazi, walikuwana juhudi ya kwendelea mbele, walikuwa wanajitoa kwa kiasi kikubwa lakini mara gafla wameacha, bidii haipo.
  5. Anafanya watu kuwa vipofu wasione kama adui  ni ndio anayesababisha hayo yote.
Adui wa ndani ni lazima aangamizwe, vita vyetu ni vya kiroho lakini siku za leo watu wamekuwa busy sana na mambo yao, hawana hata muda wa kuomba wala kusoma Neno. Kila mahali kuna adui wa ndani kazini kunaweza kutokea adui wa ndani lakini simamia Neno la Mungu hivi ni vita vya kiroho kesha katika kuomba, adui wa ndani ni mbaya mno anadhoofisha mafanikio yako analeta mvulugano unashangaa tu kutokuelewana kunatokea nyumbani kwako au ofisini kwako.
 
Shughulika na adui wa ndani sio kwa jinsi ya nyama mtakaa vikao na vikao hamtapata suluhisho huyo ni adui wa ndani kaa na mMungu yapasa umshunde chukua silaha ya Bwana mpinge huyo, adui wa ndani aliingia hata wakati wa Ibrahim akaleta migogoro katika wafanyakazi wao wakatengana, lazima usimame kupinga maadui wa ndani. Mwambie Yesu akupe neema ya ushindi uweze kushinda vita ya adui.

No comments:

Post a Comment