Ukristo una muhuri mmoja tu, ambao ni wa ROHO MTAKATIFU ndani ya mtu. Mkristo ambaye hana ROHO MTAKATIFU anatekwa kirahisi. Bila ROHO MTAKATIFU kanisa linaingia katika machafuko;
• uzinzi Kanisani na ndani ya huduma kanisani.
Watu kupeana mimba au mimba nje ya ndoa au washirika wao kwa wao kuzini kwenye kwaya au huduma.
• uchawi kuingia Kanisani.
Dalili za kifo cha kiroho ni:
1) Kukosa bubujiko la ROHO MTAKATIFU ndani ya mtu binafsi.
2) Kiwango cha kumtangaza YESU kinashuka kwa mtu binafsi.
3) Kukosa muda binafsi na MUNGU. Ebrania 10:25
4) Kuinuka roho ya ubinafsi.
5) Neno la Mungu linapoteza maana kwa mtu husika. 1 Korintho 1:18-19
6) Kuingia kwa hali ya uvugu vugu Kanisani. Yohana 4:14 -16
7) Wimbi kubwa la upotofu. Yaani wahubiri wa uongo. Kolosai 2:8,Efeso 5:6. Mahubiri yanakuwa sio kwa lengo la kumuinua Kristo bali ni juu ya utukufu wa mtu binafsi.
8) roho ya kutanga tanga kwa mpendwa. Mkristo anaanza kupenda kutanga tanga na hii ni kwasababu watu hupenda mafanikio ya mwili na sio mafanikio ya kiroho. Jinsi ya kupima mahali au kanisa kama lina Mungu wa kweli au lah;
- Je huyo mchungaji ana mzungumziaje YESU KRISTO au huko wanapoenda wanamzungumziaje YESU KRISTO?
- Je wanazungumziaje maisha yao binafsi hasa kuhusu dhambi?. Wana kemea dhambi?
- Je wanachukuliaje au wanaongeleaje kuhusu kurudi kwa YESU?
- Wanachukulia kwa uzito gani kurudi kwa YESU?
9) Kupotea ujasiri wa wokovu na kuhudumu katika nyumba ya MUNGU. Ebrania 10:35.
Dhambi inapoteza ujasiri wa wokovu. Dhambi inapoteza ujasiri wa kuhudumu na kusimama madhabahuni.
10) Kupotea kwa mamlaka ya ki MUNGU kwa mtu binafsi. Mamlaka ya ki MUNGU ikipotea na kiroho cha mtu kinashuka. Mamlaka ikipotea, mtu anakuwa ana compromise na dunia. Anakuwa hana ujasiri wa kukataa jambo baya au yasiyo sahihi mbele za MUNGU.
11) Kupoteza kwa roho ya unyeyekevu na kuinuka roho ya kiburi ndani ya maisha ya mwamini. Ezekiel 16:1 - 14, Kolosai 3:12
Karama ambazo mtu kapewa na MUNGU katika utumishi, mtu huinuka na kuwa na kiburi nazo mfano uimbaji, mziki au huduma nyengine. Mtu unapoinuliwa au huduma inapopanda lazima mtu huyo azidishe unyenyekevu. Yesu aliweza kutembea juu ya maji lakini hakumnyima Petro alipoomba na yeye kutembea juu ya maji.
12) roho ya kusahau mahali BWANA alipo kutoa. Ezekiel 16, Efeso 2:1
13) Kufanya kazi ya MUNGU kwa mazoea. Mtu kuona hana haja na kujifanya anajua zaidi katika hali ya kuleta majigambo. Mtu kutopenda kujishusha na kusema yupo level ya juu sana ya ki roho na kuwa hana haja ya kujifunza au kujishuhulisha na mambo yanayoonekana kuwa ni madogo.
14) Kuhoji na ku challenge mamlaka ya Kanisa au mamlaka ya wasimamizi wake. Mfano kumkebehi, kumsengenya au kumsema mchungaji Kanisani.
Wapo watu waliofanya hivyo na walipata madhara kwani MUNGU aliwashuhulikia kwa ku challenge, kukebehi, kumdharau mtumishi wake aliyemwita. MUNGU anaheshimu wachungaji na watu walioitwa kwa ajili ya utumishi wake madhabahuni.
Wapo watu wanasema mchungaji hana haja ya kujua maisha yao binafsi, mfano ushauri juu ya maisha ya uhusiano, uchumi,n.k. Mchungaji ana mamlaka ya ki MUNGU hata katika maisha yako binafsi, inabidi kumheshimu.
No comments:
Post a Comment