''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, September 11, 2016

ISHI KWA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

Mhubiri: Mch.Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Warumi 8:12-17
 
Ukombozi wetu upo katika kuishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Nguvu ya Roho Mtakatifu ndio itakayokupeleka katika kuishi maisha ya Utakatifu lakini usipoishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu utafanana na watu wa mataifa. Unaweza ukafanya yote wafanyayo watakatifu wa Bwana lakini inawezekana ukawa sawa na mataifa kwa kutoishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
 
Tamaa za dunia zinakujilia kwa kasi kubwa na kukushinda kwa kuwa huna nguvu ya Roho Mtakatifu na wala huishi ndani ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Tukiyafuata mambo ya mwili tunarudi katika utu wa kale kabla ya Bwana kutuokoa. Hutaweza kuyafisha matendo ya mwili wa nje ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Mtumishi wa Mungu Paulo aliwaonya WARUMI kwa habari ya kuishi maisha ya kumtegemea Roho Mtakatifu.
 
Maisha yakiwa nje ya Roho Mtakatifu utaishi kinyume na mapenzi ya Mungu. Itakuwa ni makosa makubwa sana ikiwa utaishi nje ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Maisha yenye faida ni maisha ya kuishi ndani ya Roho Mtakatifu. Kuishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu unaweza ukakosewa lakini pamoja na mateso utakayoyapata utakuwa  ni wewe na Roho Mtakatifu na wala hautakuwa wewe peke yako. Kama haujajazwa nguvu ya Roho Mtakatifu unayo kila nafasi ya kumpata Roho Mtakatifu kwa kuwa na kiu nae na kusoma Neno la Mungu kila siku.
 
HITAJI LAKO KATIKA KUISHI KWA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU
1.Kuzika Utu Wa Kale Kwa Toba
2.Kuiheshimu Kazi Ya Msalaba Ya Ukombozi wa Yesu Kristo(wagalatia 2:20)
3.Zingatia Sheria Ya Roho Wa Uzima wa Yesu Kristo(Wagalatia 3:11)
 
Baada ya kuokolewa  wewe tena si wa Dunia Hii,kumbuka kuishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Hutaweza kupata ujasiri wa Yesu Kristo ikiwa unaishi Maisha yasiyo kwa nguvu ya Roho Mtaktifu.

No comments:

Post a Comment