Mhubiri: Mch. Nelson Kazimoto
Maandiko: Mathayo 2:7-13,16,21-36, Yeremia 1:4-11, Waamuzi 13:1-2
Kila mtu hapa duniani ndani mwako kuna kusudi ambalo Mungu ameliweka ili ulitimize, sasa kwasababu hilo kusudi linalenga kuujenga ufalme wa Mungu na kuharibu ufalme wa shetani, shetani huwa analipiga vita sana; shetani atakuletea vita sana ili usiweze au usipate mpenyo/nafasi ya kutumiza kusudi la Bwana ulilowekewa ndani mwako.
Kwenye Mathayo 2:7-36, tunaona kwamba Yesu alianza kupigwa vita tangu alivyokuwa tumboni Yusufu alitaka kumuacha Mariamu,lakini pia alivyozaliwa mfalme Farao alitaka kumuua, kwanini ilikuwa hivyo? kwasababu adui alitaka kuzuia kazi ya Mungu, alitaka kuzuia kusudi la Bwana la kuwakomboa wanadamu.
Vita uliyonayo ni wasababu la kusudi ulilonalo ndani mwako, upanga mipango yako lakini unaona haiendi, umeomba sana kwa Mungu lakini unaomba hamna jibu hiyo ni vita! wachawi wanakamata ufahamu wa watu ili usiweze fanikiwa, wanatupa mapepo yafunge biashara zako ili ziharibike hiyo ni vita! Kemea kwa Jina la Yesu aliye hai! Ukiona mambo yako hayaendi ujue hapo kutakuwa tu na kitu kinachozuia, kutakuwa tu na nguvu ya shetani inayozuia kwahiyo usinyamaze kimya na kusema labda ni mapenzi ya Mungu kwako kwamba uteseke hivyo, Hapana! Mungu hajataka uteseke, amua kuingia kwenye maombi ya vita! vita vyetu si vya nyama bali ni vya kiroho. Funga na kuomba ukemee hizo roho chafu zinazozuia.
Kuokoka ni hatua ya kwanza, hatua ya pili ni kujinasua kwenye kila kifungo ulichowekewa huko nyuma, kuna wengine wamefungwa kupitia vitovu vyao, au labda umeonewa wivu na mtu akaamua kukufunga ili usiendelee mbele, ili usipate watoto, ili usioe/usiolewe, ili usifaulu darasani, ili usipate kazi, ili biashara yako ife, ili ugonjwa usipone. Habari nzuri ipo kwa ajili yako kwamba Mungu anaweza yote! wala hakuna la kumshinda, anza maombi ya vita, funga na kuomba, kemea kila roho chafu zinazozuia mafanikio yako zitoke kwa Jina la Yesu aliye Hai! usiku amka uombe, vita ni vita! hakuna kushusha silaha mpaka uone umeshinda! Usikate tamaa, jitie nguvu katika Bwana pigana! kemea hizo roho nazo zitaondoka kwa Jina la Yesu aliye hai.
No comments:
Post a Comment