UJUMBE: TUJIFUNZE UMISHENI NA MTUME PAULO NA BARNABA
MHUBIRI: Mchungaji Mhini
Maandiko: Matendo 13:9, matendo 13:3-5
Maandiko matakatifu ndiyo muongozo wetu. Paulo Mtume,
tunajifunza kwake jinsi alivyotumwa na Mungu kupeleka Injili ya Yesu Kristo kwa
mataifa. Kanisa la Umisheni ni kiini cha Umisheni na lile la Antiokia.
Kutoka mwanzo ni dhahiri kwamba, Mungu anaandaa watenda kazi
kupitia kanisa mama kuwa na maono ya kupeleka Wamishenari na vipaumbele vyote
husika. Kwamba katika Umisheni, pia lazima roho ya uvumilivu iwepo na kutiwa
moyo.
Ushindwa umehakikishwa, kwani Bwanaa Yesu mwenyewe ameahidi
kwamba talijenga kanisa lake na milango ya kuzimu haitalishinda (Mathayo
16:18).
Wakati ambapo mambo mengi yamebadilika, siri ya kuhubiri
Injili, kimsingi ni zile zile za awali zilizotumiwa na Mitume, akina Paulo na
Barnaba. Walipokuwa wakiabudu na kufunga, wakapata wito wa kumtumikia Mungu,
kwa njia ya Roho Mtakatifu, akiwaongoza, Umisheni ukaanza. Tukikumbuka kwamba,
Mungu hawaiti waliofuzu bali kuwawezesha walioitwa. Paulo na Barnaba walikumbwa
na upinzani mkali lakini hawakukata tama. Wayahudi walipowafanyia vurugu na
ghasia, Bwana aliwaambia wakung’ute mavumbi na kuwageukiaa mataifa (Matendo 13:47-52).
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kuhuburi Injili ya Yesu Kristo-katika
maana mbalimbali.
1. Nguvu ya Roho Mtakatifu, inahitajika sana ili kunena Neno
la Mungu kwa ujasiri, ishara na maajabu kutendeka.
2. Kuzifanya imara roho za wanafunzi na kuwafanya wakae
katika imani ya Neno waliloliamini (Matendo 14:22a).
3. Imetupasa kuwatia moyo Wakristo wapya kwamba, imetupasa
kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi (Matendo 14:22b).
4. Yatupasa kuchagua wazee kwa kanisa jipya lililofunguliwa
chini ya uongozi wetu kwa kufunga pamoja na kuomba (Matendo 14:23)
5. Kuwapenda watenda kazi waliopotoka mwanzoni, kwaleta
faraja ya utumishi. Barnaba alikuwa ni Mtume wa faraja kwa Yohana Marko
(Matendo 15:37).
6. Hatua ya kwanza ya kufungua makanisa, lazima ifuatiwe na
hatua ya pili ya kuyatembelea na kuyatia moyo makanisa machanga (Matendo 15:36).
Mch. Mhini (kushoto) akihubiri |
No comments:
Post a Comment