''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, May 30, 2016

MSAMAHA

Mhubiri: Mch.Kiongozi, ABDIEL MHINI
Maandiko:Mathayo 18:21-22

 "21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
 22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini".

Sisi wote ni matokeo ya msamaha. Ni wajibu wako kumsamehe yeyote anayekukosea. Kama husamehi wanaokukosea basi unafanya dhambi. Na hiyo itakuwa ni kupoteza nafasi ya kuingia mbinguni kwa sababu usiposamehe wengine Mungu naye hatakusamehe.


 Uchungu ni dhambi kubwa, unapokuwa na machungu unapata hasira, Biblia imesema sio tabia ya watakatifu. Usiwe na uchungu au usiweke machungu ndani ya moyo wako bali samehe kila anayekukosea ili Mungu naye akusamehe. Kumbuka Mungu anasamehe watu wote hivyo na wewe mtoto wake unatakiwa kufuata njia yake kwa kusamehe wote walio kukosea.

Waefeso 4:31-32
" 31 Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
 32 tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi".

Huwezi ukapata wokovu kamili kama una uchungu ndani yako. Nakukumbusha ili "USIKOSE MBINGU KWA SABABU HUJASAMEHE", iwe kazini au nyumbani kwako au mahali popote pale samehe wanaokukosea.

Mathayo 18:15
" 15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo".

Yesu anamwambia, Samehe saba mara sabini. Usitengeneze uchungu ndani ya moyo wako na kwa mtu yeyote yule.

No comments:

Post a Comment