''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 17, 2016

HUWEZI KUFICHA DHAMBI

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo
Maandiko: Yona 1:1-17
 
Kusudi la Mungu siku zote ni kuwaokoa watu wake na kuwaponya watu wake, hata kama wametenda kosa kubwa kiasi gani. Hivyo alimwambia Yona aende mji wa Ninawi kuwaambia watu wake watubu na kuacha uovu wao lakini Yona alikataa kwenda na kuamua kwenda Tarshishi, yeye mwenyewe aliamua kukimbia uso wa Mungu. Wapo watu ambao Mungu Anataka kuwainua lakini wanakimbia uso wake na kutomtii Mungu.
 
Yona alifikiri kwamba anaweza kujiepusha na uso wa Mungu na alifikiri kuwa anaweza kuishi mbali na Mungu. Inawezekana umeamua kwa makusudi kuishi mbali na uso wa Mungu. Yona akaamua kulala usingizi ndani ya melikebu iliyokuwa ikienda tarshishi akijua hatoonekana, lakini wakiwa safarini bahari ilichafuka sana na melikebu ikaanza kuyumba yumba, ndipo alipopatikana amelala. Unapoukimbia uso wa Mungu hakuna atakayejua bali wewe mwenyewe  unafahamu nafsini mwako ulicho mkosea Mungu. Ni lazima uamue mwenyewe kwa hiari yako kwamba utaishi maisha matakatifu.

Hakuna dhambi kubwa wala ndogo kwa sababu ya dhambi ni dhambi tu, Mungu atakuangamiza. Je, Mtu akimkosa Mungu ni nani atasimama ili apate kutetewa?

Yona akasema mimi siwezi kwenda ninawi. Alionyesha ukaidi kiwango cha juu, Mtu wa Mungu acha ukaidi na ukaitii sauti ya Mungu, Utii Maagizo Ya Mungu.
 
MADHARA YA DHAMBI
-Inaleta kifo cha kimwili na kiroho.( Mithali 6:32)
-Inakutenga Mbali Na Uso Wa Mungu.
-Inaleta majeraha yasiyofutika.
-Inaleta Fedheha Na Kuondoa Heshima.
-Inaleta Mateso.
-Inafanya Usifanikiwe kwa Jambo lolote.

Achana na dhambi, unaweza kuifurahia ukaona ni nzuri lakini mwisho wake ni mbaya sana. Dhambi lazima ipatilizwe ili tuweze kwenda salama na Mungu. Ili usiishi maisha ya dhambi tena ni lazima uichukie na kumuomba Mungu hapo ndipo utakuweza kuiacha. Iko nafasi ya kumrudia Mungu. Yona alipoulizwa ili bahari itulie kitu gani kilitakiwa kufanywa alisema kuwa, "Nikamateni mkanitupe baharini nayo itatulia". Mungu aliye hai ndie Yeye pekee anayepaswa kuabudiwa. Rudi na ukatubu dhambi zako ukaanze upya na Mungu.
 
Je,Kipimo cha Mungu kikipita una ujasiri wa kusimama mbele za Mungu na kusema lolote?Using'ang'anie dhambi maana Mungu hapendezwi nayo, simama na ukatubu dhambi zako zote.

No comments:

Post a Comment