''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 3, 2016

MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: Waefeso 1:15-19
 
 Kutiwa nuru macho yako ya rohoni. Kama binadamu tuna milango ya fahamu na mmoja wapo ni macho lakini hapa ujumbe wetu hauongeli macho ya mwilini bali macho ya rohoni. Tuliposoma Mtume Paulo alikuwa anawaombea watu wa Efeso ili macho ya mioyo yao yatiwe nuru.
 
Kabla hatujaokoka macho ya mioyo yetu yanakuwa yako kwenye giza kwasababu yanakuwa hayawezi kuona chochote katika ulimwengu wa roho, kwahiyo unapookoka macho ya moyo wako yanaanza kupata nuru. Lakini kumbuka kwamba tunapoongelea macho ya moyoni tunamaanisha "uelewa wa kindani  sana wa Mungu au uelewa sahihi sana wa ki-Mungu" tunaongelea uwezo wa kuona kupitia Mungu. Haumuelewi Mungu kwasababu umesoma sana biblia mpaka chuo bali utamuelewa kwa kupitia macho ya moyoni yaliyotiwa nuru na nuru hiyo ni Yesu mwenyewe.
 
Unapo okoka Yesu ambaye ni NURU anaingia moyoni mwako ndipo macho yako yanapoanza kupata uwezo wa kuona na lile giza la macho ya moyoni linaondoka pole pole unavyozidi kuwa na ushirika wa karibu na Mungu mpaka unaanza kuona vizuri kabisa kwenye ulimwengu wa roho. Kabla hujaokoka unakuwa huoni kabisa katika ulimwengu wa roho hata ukiambiwa Roho Mtakatifu unakuwa humuelewi.
 
Nuru ya macho ya moyoni ni ya muhimu sana sana kwasababu bila hiyo hutaweza kuona wala kuelewa kitu kinachoendelea katika ulimwengu wa roho. Lakini sio hivyo tu bali pia hutaweza kumuelewa Mungu kwa usahihi. Pia Nuru ya macho ya moyoni inatuwezesha kuelewa tumaini la mwito wetu, tumaini la mwito wako kama mtu uliyeokoka, tumaini la wito wako kama mtumishi wa Mungu, ndomana Mtume Paulo alisema "...ili mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo..". Kwahiyo nuru ya macho ya moyoni ni ya muhimu sana. 

No comments:

Post a Comment