MHUBIRI: MWINJILISTI GREYSON NYANTAMBA
Maandiko: Mathayo 14:15-21
Maandiko: Mathayo 14:15-21
Yesu alijitenga na kwenda nyikani lakini wanafunzi walipata taarifa na makutano nao wakamfuata maana walipenda kusikia kutoka kwa Yesu. Na kwa sababu hiyo ilikuwa kiu ya mioyo yao wakamfuata na wengine wakamtangulia. Biblia inasema Yesu alipofika akawakuta makutano waliomtangulia na Yesu akawahurumia. Unaweza usijue maana ya nyikani, Nyikani ni sehemu isiyo na kitu chochote bali kuna vichaka vidogo vidogo, kwa jina lingine tunasema ni jangwani. Jioni ilipofika Biblia inasema wanafunzi wa Yesu walimfuata Yesu na kumwambia kuwa makutano wanahitaji kula na kunywa. Yesu akawajibu na kuwaambia kuwa "Wapeni nyinyi chakula". Na hivyo ndivyo Yesu anavyosemaga, wakati huna kitu ndio anakwambia nipe. Makutano wakasikia kuwa Yesu amewambia wanafunzi watoe chakula. Lakini wanafunzi wa Yesu hawakuelewa kwamba watatoa wapi chakula cha kuwapa makutano hao.
Nataka nikuambie ndugu yangu "Lisolowezekana kwa wanadamu kwa Mungu linawezekana". Suluhisho la Mungu halipo katika fedha tu bali Mungu ana njia zake nyingine nyingi. Wakati mwingine Yesu anaposema huwa tunatazama tulivyo navyo na hapo ndipo tunapofanya kosa. Wanafunzi wakamwambia Yesu kwamba hawana chakula cha kuwapa makutano. Mungu anafanya kwa wakati wake na kwa njia zake mwenyewe na akisema amesema.
Hatima ya jambo lako itakuja kwa kuweka jambo au shida yako mikononi mwake na ukiweka mikononi mwake hakuna jambo litakaloharibika. Pamoja na makutano kusikia wanafunzi wa Yesu kujibu kuwa hauna chakula cha kuwapa makutano hawakukata tamaa bali waliendelea kumsikiliza Yesu. Usisikilize wanadamu wanasema nini juu yako au juu ya jambo lako bali msikilize na kumtazama Yesu aliye hai. Wakati mwingine watu wanaweza wakakutazama kama mtu uliye shindwa, wewe usiangalie mtazamo wa wanadamu hao bali mtazame Yesu pekee.
Wanafunzi wa Yesu wakamwambia Yesu kwamba kuna samaki wawili na mikate mitano kwa mtoto. Mtoto yule alitoa mikate yake na samaki wake ili makutano wapate chakula. Usijione Mnyonge Bwana atakuwezesha, usikate tamaa. Yesu akachukua ile mikate na kuiombea na makutano walikula hata kusaza. Ukijitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa Yesu hautopata hasara ya aina yoyote bali baraka tele kutoka kwake.
KINACHOAMUA HATIMA YAKO NI NENO LA MUNGU LILILO NDANI YAKO. Haijalishi umepita katika mapito ya namna gani Mungu anaweza kukufungua na vifungo vyako vyote.
Amina
ReplyDelete