Neno: 1 Yohana 2:15-16
Yohana anatukumbusha kwamba tusiipende dunia, mfalme wa hii dunia ni shetani. Labda kabla ya kwenda mbali tuangalie mtu aliye na Mungu ni nani, Mtu aliye na Mungu ni yule ambaye amempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na anamuheshimu Mungu na kufanya yale yote anayotaka Mungu.
Acha acha kabisa kuipenda dunia. Tatizo la kanisa sasa ni kujichanganya na dunia, kuchanganya vitu, inawezekana unakaa na watu ambao hawajaokoka, sasa usipokuwa makini unaweza ukarudishwa nyuma ukajikuta muda mwingine unakubaliana na baadhi ya mambo yao ya dunia. 1Yoh 2:6 inabidi tuenende kama Yesu. 1Yoh 1:5-6 giza ni giza tu usipende giza hata kidogo, kma unampenda Mungu enenda kama Yesu anavyokutaka uende, enenda kama Yesu. Wewe ni mtu wa Mungu achana na mambo ya dunia, acha kuhalalisha mambo ya kidunia yasio mpendeza Mungu kuwa kama yanayo mpendeza Mungu.
Vidokezo Muhimu
1. Kuamini ukweli wote, ni lazima uwe una tabia ya kusoma Neno la Mungu mara kwa mara na kuliamini kwa dhati.
2. Tambua sayansi na mifumo ya dunia ni ya muda tu na itakuja kufika mwisho lakini roho yako inaishi milele kwahiyo angalia unaiandaaje roho yako kwa ajili ya maisha ya badae, Dan 2:34-35. Vitu vinaweza kuwa vinavutia katika macho yetu lakini kama vimekatazwa na Mungu achana navyo tu, nakuonya mtu wa Mungu kuwa makini na dunia shetani ni mjanja sana na ana njia nyingi mno bila kuwa makini unaweza ukajikuta tayari umeingia kwenye mtego, umefanya dhambi. Wewe kama mtu wa Mungu ni lazima uamue kuishi maisha matakatifu, ni uamuzi lazima uamue kutoka ndani.
3. Lazima ukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu, wewe kama mtu wa Mungu kuwa na mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu na taka sana kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Kuwa makini sana na watu wanaokuzunguka marafiki zako wanaweza kukushauri kufanya kitu flani, kama uko chuo wanaweza kukushauri twende sehem flani ya starehe lakini jitambua wewe ni nani na linda utakatifu wako sana. Wengine unajikuta unapenda sana kuangalia vipindi vya tv ambavyo ni vibaya havimpendezi Mungu, ni afadhali ukaamua kuacha kabisa maana vile vitu vinakupunguzia kasi yako ya kuishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu.
No comments:
Post a Comment