''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 17, 2018

USIMKIMBIE MUNGU

Mhubiri: Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Yona 1:1-15

Yona alitumwa kazi na Mungu ya kwenda Ninawi lakini akaamua aikimbie ile kazi kwa kukimbilia Tarishishi. Na sisi katika maisha ya leo, huwa kuna hali mbalimbali au kuna wakati huwa tunamkimbia Mungu. Mungu anakwambia kitu lakini unakwepa kufanya kazi aliyokuagiza na kwenda kufanya mambo yako. Kila mtu ana maisha ya tofauti lakini Mungu amekupa maisha hayo na mahali ulipo kwa kusudi maalum, kwa kusudi fulani la kufanya, katika mazingira hayo hayo ulipo. Katika mazingira hayo ulipo, Mungu amekupa kazi ya kufanya, sasa Je unaikimbia kazi uliyopewa na Mungu kama Yona alivyofanya au unaifanya?

Hapo Yona alipokuwa anakimbilia kulikuwa ni mbali sana, ile safari ilikuwa ichukue siku nyingi, kwahiyo sio kwamba alienda kimakosa bali alipanga kabisa labda kwenda kutafuta biashara. Hiyo ni kama sisi pia huwa tunazani kuliko kutimiza lile lengo la Mungu alilokupa ulifanye hapa duniani, unawaza kutimiza malengo yako kwanza. 

Kwenye mstari wa 4-5: "Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi."

Angalia hapa madhara unayopata unapomkimbia Mungu au kazi ya Mungu. Kumkimbia Mungu husababisha matatizo kwako au kwa familia yako nzima ambayo wao hawakuhusika lakini utawaletea matatizo. Yona akasababisha abiria wote na wao wapate shida.

Tambua kuwa Mungu amekuleta hapa duniani ili ufanye kitu kwa niaba yake, kwahiyo usimkimbie Mungu wala kufanya kazi zake. 

No comments:

Post a Comment