''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, January 21, 2013

MADHARA YA USINGIZI WAKATI WA HATARI
--------------------------------------------------

Huo ndio ujumbe wa jumapili uliofundishwa na Mch. Peter Mitimingi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Neno lilikuwa, Mathayo 13:24-25, Mchungaji alikazia katika dondoo 3 za muhimu


1. Watu wanapolala ndipo adui anapoanza kazi zake za uharibifu. Mpanzi alipolala ndipo adui alipopata nafasi ya kupanda magugu katika shamba lake. Adui alisubiri mpaka mpanzi alipolala ndipo akapanda mbegu mbaya, shetani anasubiri mpaka ulale kiroho ndipo apande mawazo na roho chafu moyoni mwako. Usipokuwa makini shetani hung’oa na kuharibu Neno la Mungu lililokuwa ndani mwako.

2. Shetani anasubiri unapolala ndio afanye kazi zake, shetani hana uwezo wa kupora haki zako mchana wakati upo macho. kwahiyo atakubembeleza na kukutengenezea mazingira mazuri ya wewe kulala ili apate nafasi ya kuharibu maisha yako, 1 Wafalme3:20. Kama utakuwa hai kiroho shetani kamwe hataweza kukuibia haki zako.

3. Kanisa la Mungu Tanzania linasinzia na kumpa nafasi shetani ya kuliibia, watakatifu wengi sasa wamekuwa wavivu kuomba na kusoma Neno la Mungu, wengi sasa wamekuwa wakijali kazi na biashara kuliko kumtafuta Mungu. Acha kumpa nafasi ibilisi, badilika sasa ili uiokoe Tanzania na zaidi ya yote ufike Mbinguni.


ANGALIA VIDEO YA MAHUBIRI


 
Wanafunzi wa Alpha sec school wakisikiliza Neno la Mungu


No comments:

Post a Comment