''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 6, 2013

JIHADHARI NA MAFUNDISHO POTOFU

MAANDIKO: 2Timotheo 3:1-5, 1Timitheo 4:1-2, 1Yohana 2:18-29, Matendo 20:28-30
Mhubiri: Mch. Peter Elias
  
Mafundisho potofu huaribu fahamu za watu, kwahiyo kuwa makini sana na mafundisho ya siku hizi. 
Paulo anaposema hatari ni hatari kwa kanisa au mtu uliyeokoka kwasababu kwa mtu asiyeokoka hayo mambo si hatari, kama kutukana, kuzini sio hatari kwa mtu ambaye hajampokea Yesu lakini ni hatari kwa mtu aliyeokoka. Yesu alisema siku hizi ni za hatari alimaanisha hatari kwa mtu mtakatifu kwahiyo kuwa makini sana na mafundisho mbalimbali hata kama ni ya kanisani kwako

Kizazi cha sasa kimebadilika sana kimekuwa na tabia chafu, shetani anakamata fahamu za watu anawapa elimu yake chafu, watu sahivi wanaona kuvaa suruali inayobana ni vizuri lakini kumbe wamepotea. Sahivi kuna mifumo mingi ya mafundisho ya kishetani, pia hata kwenye haki za binadamu kuna mafundisho ya kishetani kama kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana wakati imekatazwa kabisa kwenye biblia. Sasa kumejaa mafundisho ya uongo mafundisho ya mashetani,na mafundisho ya kupenda fedha, na roho za kupenda fedha zimekidhiri mno. Unapofundisha mambo ya fedha ni lazima uwaambie watu jinsi ya kuzitumia fedha hizo ili wasimtende Mungu dhambi lakini watumishi wengi hawafundishi hilo kwasababu wamejaa tamaa ya hela.

  Watu wengi sasa hawasomi biblia ndomana wanadanganyika haraka na kirahisi, likisemwa neno huwezi kujua kama ni la kutoka kwa Mungu au lah kwasababu hauna msingi wa Neno la Mungu. Hauwezi kugundua tapeli kwa akili zako tu bali utamgundua kwa Roho Mtakatifu, amani ya Kristo iamue moyoni mwako na sio akili zako lakini kama moyo wako uko wazi yaani hauna Neno la Mungu ndani mwako hautaweza kujua kabisa kama unadanganywa. 

Ukitaka kufanikiwa fuata yale anayokuambia Mungu, amesema ukifuata kila kitu anachokuagiza hivi leo utafanikiwa mjini utafanikiwa mashambani. Penda sana kusoma Neno la Mungu, Neno la Mungu likijaa ndani mwako kwa wingi na ukawa na Roho Mtakatifu utaweza kutambua roho,  pia uwe na mfululizo mzuri wa maombi.Amen.No comments:

Post a Comment