''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, December 15, 2013

KANUNI 5 ZA KUTAWALA..

MHUBIRI: Mch. Sanga
Maandiko: Mwanzo 1:1-13,Ezekiel 37:1-8

1. LAZIMA UWE NA WAZO (VISION)
 Mungu alianza na wazo la kutengeneza dunia na badae alitamka  na kuiumba dunia na vyote vilivyo ndani mwake. Kulikuwa na wazo ndani ya moyo wa Mungu la kuiumba dunia.

Watu wengi leo wanataka kuendelea lakini hawana wazo la kuendelea. Ni lazima uwe na wazo la kuendelea kwanza ndipo utaweza kuendelea, hata misaada ya nje ya nchi haitolewi mpaka uwe na wazo la kufanya. Na wengi husema pesa ndio msingi wa maendeleo lakini ukweli ni kwamba pesa siyo msingi wa maendeleo kama huna wazo au lengo au maono. Mungu alianza wakati juu ya uso wa nchi hamna kitu akaanza kutamka, pia katika kitabu cha Ezekiel Mungu alimuuliza ezekiel unaona nini akasema anaona mifupa, akaulizwa je mifupa hii inaweza kuishi?, lakini badae Mungu alimwambia atabiri juu ya mifupa ile, mifupa ile ilikuwa haina kitu lakini Mungu aliona jeshi katika mifupa ile. Kwa kawaida Mungu humletea mtu kwanza maono, yale maono ndiyo yanaanza kufurukuta ndani ya moyo ya mtu na baadaye huleta mpango kamili wa kufanikisha wazo hilo. 

2. WEKA MPANGO WA KUTIMIZA WAZO LAKO. 
 Ni lazima uwe na mpango, maono yanatengeneza mpango, Mungu alimwambia ezekiel tabiri, kile kitedo cha kutabiri hakikuwa cha mara moja bali alipoamini na kuthubutu kuanza kutabiri alipoendelea na kuendelea mpaka likawa jeshi kubwa

 3.LAZIMA UPATE au UTAFUTE UFAHAMU YA ULE MPANGO ULIONAO
 Ezekiel akaambiwa endelea kutabiri, Mungu alimwambia ibrahim atampa uzao mkubwa wakati kwa muda ule alikuwa hana mtoto wowote lakini alipokea wazo lile, lakini lile wazo lilimpa kuwa na mkakati na ufahamu wa kutimiza. 

4. TUMIA KILA FURSA ILIYOPO ILI KUTIMIZA WAZO AU MAONO ULIYONAYO. 
Lazima kama mtu wa Mungu utumie kila fursa Mungu anayokupa mbele yako, jitaidi kutumia vizuri fursa uliyonayo. Ukarimu wa ibrahim ulimpelekea yeye kupewa fursa baada ya kuwakaribisha wale malaika. Mungu amekupa fursa ya kusoma, kuwa kazi, au kuwafanya biashara, tumia hiyo fursa vizuri sana. Mungu anapoileta fursa inakuwa na majira yake kwahiyo ukiiacha itapita bila kuitumia, kwahiyo itumie vizuri ili inapopita usijutie kupita kwa iyo fursa. 

5. TATHIMINI KILE ULICHO KIFANYA. 
Je nguvu uliyonanyo na kile ulicho kifanya vinafanana au havifanani?, kuwa na uwezo wa kutathimini kile ulichokifanya. Je, kile ulichokifanya ni sawa na Neema ya Mungu aliyokupa?. 

LAKINI YOTE JUU YA YOTE, YALE ULIYOYATAZAMIA KWA MUNGU ATAYATEKELEZA KWA WAKATI WAKE, MUNGU ANAHESHIMU SANA WATU WENYE MAONO NAYE NA MAONO YA WATU WAKE, LAZIMA UWE NA MAONO KWA AJILI YA MUNGU NA MAONO KWA AJILI YA MAISHA YAKO.

No comments:

Post a Comment