''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 18, 2015

HATARI YA KUTOKUWA NA MOYO MNYOOFU MBELE ZA MUNGU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: 2Wafalme 5:1-27

Habari hiyo ina mambo makubwa mawili(2)

1. Neema ya Mungu inavuka mipaka yote bila kujali huyu kabila gani , ndio maana mpaka Naamani ambaye hakuwa muisrael alipata Neema hiyo, Neema ya Mungu inampata yeyote Mungu anapotaka.

2. Hukumu ya Mungu kwa mtu aliyevunja masharti ya Mungu, ipo hukumu ya Mungu ya wasio fuata maagizo ya Mungu.

Naamani analikuwa na sifa tatu, Alikuwa Mkuu mbele za Bwana wake, Alikuwa hodari wa vita Alikuwa ni hodari lakini ukoma ulikuwa kama ni kikwazo lakini siku moja kupitia mjakazi wake neema ya Mungu ilimshukia na kumponya ukoma wake.

Naamani alienda na zawadi mbali mbali kwa ajili ya kumpa nabii Elisha kwasababu ya kuponywa kwake, lakini nabii Elisha alikataa kabisa kuchukua zile zawadi kwasabau aliyemponya ni Mungu na sio yeye mwanadamu. Lakini gehazi mtumwa wake nabii Elisha alitamani zile zawadi. Baada ya Naamani kuondoka na zawadi zake, Gehazi akamkimbilia Naamani njiani, akaamua kumdanganya kuwa kuna wageni wamekuja kwahiyo bwana wake amemtuma ili ampatie talanta mbili kutoka kwa naamani.

Gehazi akaingiwa na roho ya tamaa mpaka akaanganya, yawezekana wewe unafanya kazi sehemu ambayo kuna vitu vizuri, lakini usiingiwe na tamaa ya kuchukua vitu hivyo. Tamaa ilimfanya gehazi apate ukoma. 

No comments:

Post a Comment