''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 11, 2015

NIMRUDISHIE BWANA NINI KWA UKARIMU WAKE WOTE ALIONITENDEA?


Mhubiri: Mr. Masembo
Maandiko: Zaburi 116:12-14

Mtunga zaburi ambaye ni Daudi alikaa akawaza sana mpaka akatoa maneno hayo, akamtafakari Mungu kwa undani sana akaangalia mambo yote ambayo Mungu alikuwa amemtendea  ndipo akasema maneno hayo “Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea”.
Na wewe unapomtafakari Mungu unatakiwa ufike mahali ambapo uatajiuliza umrudishie nini Bwana kwa ajili ya ukarimu wake wote aliokutendea. Mtumishi wa Mungu Daudi alifika mbali akawaza mambo yote Mungu aliyomfanyia  kwani yeye ni nani mbele za Mungu mpaka Mungu amtendee mambo mengi vile basi akawa na moyo wa shukurani mbele zake.
Mtumishi wa Mungu Daudi akaendelea kusema atapokea kikombe cha wokovu na kilitangaza Jina la Bwana. Yawezekana katika maisha yako hujaweka kuhubiri injili kama kipao mbele chako cha kwanza lakini kumbuka hilo ndilo agizo letu kuu tulilopewa na Yesu kama watu tulio okoka, unatakiwa uwashuhudie watu wengine  habari za Yesu ili na wao waje kwa Yesu. Bwana Yesu alisema enendeni mkaihubiri injili kwa mataifa yote, na hiyo ndio kazi kuu tiliyopewa, hakuna kazi Mungu anayotudai sana Zaidi ya hii kuwaambia watu habari za Yesu.

 

 

No comments:

Post a Comment