''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, July 19, 2015

MAMBO 5 YA YALIYOMTOFAUTISHA YESU NA WENGINE


1.YESU ALIONA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUONA
2.YESU ALIAMINI MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUAMINI
3.YESU ALISEMA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUSEMA WALA KUELEWA (spiritual language)
4.YESU ALISIKIA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUSIKIA
5.YESU ALIFANYA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUFANYA
 
 
JAMBO LA KWANZA
YESU ALIONA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUONA
1.        Yesu aliwaona Makutano akawahurumia. Wengine waliona makutano na wakataka warudi makwao.
Mathayo 9:36 “36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.”
Marko 6:36  Uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula.

Yesu anatutaka na sisi tuliomwamini tuone tofauti na dunia inavyoona.”
 
2.        Yesu aliona senti ya mama mjane, wengine waliona mamilioni ya matajiri.
Marko 12: 41 – 42 “41 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;”
Dunia huwaona wasio nacho kama watu wa kupuuziwa na kuwekwa nyuma, Yesu huwaona watu wasionacho kama watu wa muhimu na wakutangulizwa mbele.
 
3.        Yesu aliiona nia ya ndani ya Zakayo, wengine waliyaona maovu ya Zakayo.
Luka 19:5 - 7
5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
 
Yesu huangalia huyu ni nani kesho, wanadamu huangalia huyu alikuwa nani jana.
·         Macho ya Yesu huangalia kuona maisha ya kesho, bali macho ya wanadamu hunagalia kuona maisha yale ya jana.
·         Macho ya Bwana yanatafuta jema ndani ya mtu, macho ya wanadamu yanatafuta maovu ndani ya mtu.
·         Macho ya Yesu yalimuona Paulo wa kesho, wakati macho ya wanadamu yalimuona Sauli wa jana.
 
Paulo wa kesho:
Matendo ya Mitume 9:11
Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Sauli wa Jana
Matendo ya Mitume 9:26 “Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.”
4.        Yesu aliona maelfu ya samaki na mikate, wengine waliona mikate mitano na samaki wawili.
Mathayo 14:15 – 21
         i.            Wanadamu waliona nyika iliyojaa ukame, Yesu aliona nyika iliyojaa neema, vyakula, uponyaji wa mwili na roho.
        ii.            Yesu alikuwa anaona mikate na samaki za kula maelfu ya watu, wanafunzi walikuwa wanaona mikate na samaki za kula mtu mmoja.
      iii.            Yesu anataka uone kile anachokiona yeye kila akiyaangalia maisha yako.
      iv.            Kile anachokiona Yesu juu ya maisha yako ni kikubwa sana kuliko kile unachokiona wewe katika uhalisia wake.
        v.            Yesu anauona muujiza wako kabla haujatungwa mim
      vi.            Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
 
5.        Yesu alimuona binti wa Yairo akiwa amelala, wanadamu walimuona binti wa Yairo akiwa amekufa.
Marko 5:35 - 43
         i.            Watu walikuwa wakilia na kufanya maombolezo makuu juu ya binti wa Yairo.
        ii.            Wanadamu wanaokufanyia maombolezo juu ya kushindwa kwako, wasubiri "suprise" ya Bwana Yesu.
      iii.            Wanadamu walitangaza msiba wa binti Yairo, Yesu alitangaza uzima wa binti Yairo.
Marko 5:39
       iv.            Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.
        v.            Yesu hakusema msichana FUFUKA bali alisema msichana INUKA
Marko 5:41
41 Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.
      vi.            Wanaofikiri umekufa, waambie umeinama tu, muda si mrefu utainuka.
 
6.        Wanadamu wanakuona umebeba mimba, Mungu anakuona umebeba Mataifa. Mwanzo 25:21 - 23
                                 i.            Rebeka aliona watoto wakishindana, Bwana aliona mataifa yakishindana.
                                ii.            Wewe unaona umebeba nini? Umebeba mimba au Umebeba Mataifa?
                              iii.            Mungu anataka uone kama anavyoona yeye.
 
 

 

No comments:

Post a Comment