''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, July 13, 2015

NGUVU YA MANENO / MATAMSHI

Mhubiri: Mch Ambele Chapanyota
Maandiko: Mwanzo 22:1-8, Kutoka 2:1-9, Luka 23:24
 
Kuna Nguvu katika maneno unayotamka,iko nguvu inatoka, Mungu alitamka maneno dunia ikaumbika hakukuwa na wajenzi lakini Mungu aliongea maneno dunia ikaumbwa, na sisi ambao tumeokolewa na Yesu iko nguvu kwenye maneno yetu, biblia inavyosema mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya haimaanishi ulikuwa mlevi sasa umeacha basi au ulikuwa mpagani sasa umeokoka basi, ilivyosema umekuwa kiumbe kipya inamaanisha kuna utofauti katika kila kitu ambacho unakisema kwenye maisha yako. Kuwa kiumbe kipya sio kuacha dhambi peke yake inaamansha kuna vitu ulikuwa huwezi kufanya zamani baada ya kuwa kiumbe kipya kuna vitu unaanza kuvifanya na vinafanyika na ndio maana lazima uelewe sasa kuna nguvu katika maneno yako yawezekana zamani ulikuwa unatamka ovyo ovyo lakini sahivi wewe ni kiumbe kipya maneno yako yana nguvu inayoweza kujenga au kubomoa, maneno yako mwenyewe yanaweza kukupa 'future' nzuri au kubomoa 'future' yako mwenyewe, yanaweza kukupa mke/mume mzuri au mbaya au hata kumharibu mke/mume mzuri, vitu unavyomtamkia mke/mume wako au mtoto wako yanaweza kumbadilisha kuwa mzuri au kumuharibu.
 
Maneno yako yana utendaji, chochote unachoongea kinatendewa kazi, hakuna kitu utatamka kitaenda peke yake hapana lazima nyuma yake kuna utendaji. Mtu uliyeokoka lazima uangalie maneno unayotamka, unatamka nini kwenye kinywa chako, lazima uwe na mipaka kwenye mdomo wako sio upo kwenye jaribu kuropoka tu mara unasema 'maisha yako ni magumu tu' au 'somo hili ziliwezi' au 'biashara ni ngumu' au 'pesa ni ngumu kupatikana'. Kumbuka wewe ni wakiri wa Kristo duniani kwahiyo maneno yako yanawakilisha mbingu hapa duniani ndio maana tukisema pepo toka zinatoka, tukisema kuwe na uzima uzima unashuka maana maneno yetu yana nguvu vitu vilivyokufa vinaweza kufufuka. Maneno yako sio ya kawaida kwakuwa wewe sio wa kawaida tena baada ya kumpokea Yesu.
 

No comments:

Post a Comment