''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 26, 2015

UPENDO

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Marko 12:29-31,1Wakorintho 13:1-13
 
Kama mtu uliyeokoka unatakiwa kumpenda Mungu lakini sio tu kumpenda Mungu  bali na kumpenda jirani yako pia. Bila upendo sisi si kitu, upendo ndio chanzo cha kila kitu, muda mwingi tukihudhuria sherehe huwa tunatoa zawadi ni kwasababu ya upendo tulionao kwa huyo mtu na hivyo hivyo ndivyo Yesu alivyoonesha upendo wake kwa kutupa Roho Mtakatifu ndio maana alisema msubiri mpaka nguvu itakapo wajilia.
 
Roho Mtakatifu alikuja kwasababu ya upendo wa Yesu kwetu sisi. Yesu aliwapa watu chakula, aliombea watu ni kwasababu ya upendo ndiomana akasema hakuna amri kuu kama hii.
 
Kama utampenda jirani yako hutamsemea vibaya, hebu jikague mwenyewe kuhusu upendo, je unawapenda jirani zako? kama huwapendi jirani zako unaweza ukaenda kanisani sana ukatumika sana lakini kama humpendi jirani yako hayo yote ni bure.
 
 1Wakorintho 13:1-13 Wakorintho walikuwa wanena kwa lugha lakini bado hawapendani wao kwa wao, wanasemana vibaya, na wewe pia unaweza ukawa muombaji sana lakini usipompenda mwenzako hayo yote unayofanya ni bure.
 
Usipopenda hutakuwa mtoaji kwasababu chanzo cha kutoa ni upendo, ukimpenda Mungu moja kwa moja utatoa fungu la kumi, utasaidia watu wenye shida. Kutoa unaweza kutoa lakini kutoa bila upendo ni Buree, kutoa na upendo vinatakiwa viwe pamoja. upendo wa kweli huvumilia.
 
Ukiwa na upendo hutaweza kufanya dhambi kwasababu kama unampenda Mungu wako hutataka kumuuzi Mungu wako, Upendo hautakiwi kupungua hata kidogo katika maisha yako. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hebu jiulize ni kiasi gani unampenda jirani yako? ni kwa kiasi gani unampenda mume/mke wako? ni kiasi gani unawapenda watu wanaokuzunguka?, na kama unampenda Yesu na unampenda jirani yako basi utamshuhudia kuhusu habari ya Yesu ili aokoke na yeye.

No comments:

Post a Comment