''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, December 13, 2015

KATIKA HALI YOYOTE UNAYOPITIA, LIPO TUMAINI KWA AJILI YAKO

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo
Maandiko: 1Samweli 30:1-8,16-20; Waebrania 13:5


Hapa ni wakati jeshi la Israel likiongozwa na mfalme Daudi kurudi siklagi na kukuta familia zao zimetekwa na maadui. Wanaume ambao ni wanajeshi wakalia wakalia mpaka wakakosa nguvu ya kuendelea kulia tena. Ukipita katika hali nguvu  sawa unaweza kulia na kulia lakini hutakiwi kuishia hapo, kuna kitu cha ziada unatakiwa ufanye, lazima ufike mahali uamue kuondokana na ile hali ya kuendelea kulia, kusikitika, kujikunyata na kuamua kufanya kitu;  na kitu hicho ndicho Mfalme Daudi alichokifanya. Mfalme Daudi aliamua kwenda kwa kuhani na kumuomba naivera, aliamua kuacha kulia na kwenda mbele za Mungu na kumwambia shida yake kwa kumaanisha na baadae Mungu alijibu na hatimaye aliweza kurudisha familia zote zilizo tekwa.
 
Yawezekana umelia sana umevunjika moyo lakini tambua katika hali yoyote unayopitia jibu lipo kwa ajili yako. Acha kulia na amua sasa kumwambia Mungu, muelezee shida zako zote naye atakujibu kuendana na mapenzi yake. Ukipata shida yoyote hakuna sehemu nyingine ya kupata msaada bali ni kwa Yesu Kristo tu.

No comments:

Post a Comment