''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, December 7, 2015

KUMTUNZA ROHO MTAKATIFU KWA GHARAMA YOYOTE

Mhubiri: Mr. Mwalongo
Maandiko: Warumi 8:7-21

Historia fupi ya Roho Mtakatifu
katika agano la kale Roho Mtakatifu alikuwa akijaa kwa watu maalumu lakini katika agano jipya Roho Mtakatifu anajaa kwa wote nasi tunaiona nguvu ya Roho Mtakatifu inavyofanya kazi.

Roho Mtakatifu alifanya kazi pamoja na watu wa Kristo nao wakakanzisha makanisa kila wanapoenda kuhubiri lakini makanisa haya yanayoanzishwa hukaa kwa muda mfupi na kupotea.na hii ni kwa sababu ya watu wa makanisa haya kumwacha mungu.
Baada ya kupita miaka mingi,uamsho wa roho mtakatifu ulirudi tena.ilikuwa katika miaka ya 1900.
 
ROHO MTAKATIFU hakai mahali palipo na uchafu wa aina yoyote kwa kiwango cha aina yoyote. Ni wajibu wa kila mtakatifu,mwanafunzi wa Kristo kumtunza Roho Mtakatifu.
 
 Tunamtunza Roho Mtakatifu kwa kuwa watakatifu wakati wote. Yatupasa kumtunza Roho Mtakatifu wakati wote kwa gharama yoyote. Yapo masalia machache ya watu waliosema watamtunza roho kwa gharama yoyote na walio wengi mioyo yao imetiwa ganzi ndani yake.
"MASALIA HAYA YATAKAPOONDOKA KANISA LA MUNGU LINAGEUKA"
Hapa ndipo kanisa linaweza kugeuka na kuwa dini. Ukiona moyoni mwako hakuna kengele ya Mungu kukuonya au kukufundisha ujue Mungu hayupo ndani yako. Na hii ndiyo maana Mungu anasema
"asiye na Roho Mtakatifu huyo si wa Kristo". Je,ni jambo gani lililo na gharama ya kukutoa katika uwepo wa Mungu?
 
JE UNA KIU YA KUSOMA NENO LA MUNGU NDANI YAKO?
JE KIU YA MAOMBI BADO IPO NDANI YAKO?
 
Wapo watu wanaotafuta pesa kwa Gharama yoyote lakini sisi Yatupasa kumtunza Roho Mtakatifu kwa gharama yoyote. Tunapokuwa na Roho Mtakatifu hatutababaishwa na chochote katika dunia hii,wala si nyumba, gari, na kitu chochote. Kitu cha kwanza ni kumtafuta Roho Mtakatifu na mengine yatafuata.

No comments:

Post a Comment