''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, December 26, 2016

JE, UMEMRUHUSU YESU AZALIWE MOYONI MWAKO?

Mhubiri: Mzee Kiong. Elifuraha Mumghamba
Maandiko: Mathayo 1:18-25, Luka 1:29-33,2:9-11, Isaya 9:6, Yohana 3:16-17

Habari ya kuzaliwa Yesu imeelezewa vizuri kwenye vitabu vya injili viwili ambavyo ni Mathayo na Luka, lakini pia ni habari iliyotabiriwa miaka 700 nyuma katika kitabu cha Isaya 9:6.

Tukisoma Biblia tunatesema Mungu anaweza kila kitu lakini ukija kwenye maisha yenyewe kuna mambo unaweza ukahisi kwamba Mungu anaweza akashindwa kufanya au huelewi itawezekana vipi, labda una hali unapitia ambayo unaona haiwezekani lolote kufanyika, sasa Mariamu na yeye alikuwa anajiuliza itawezekanaje kupata mtoto wakati alikuwa hajamjua mume? lakini malaika akamwambia kwa uwezo wa Mungu atapata mimba na Mtoto huyo atamuita jina lake Yesu. Tambua kwamba Mungu anaweza kila kitu na anavyosema anaweza kufanya kitu chochote uzizani ni maneno tu bali ni kweli anaweza. Lakini pia kupitia huu muujiza uliomtokea Mariam unaweza kujifunza kwamba Mungu anafanya mambo kwa jinsi ya ajabu sana Zaidi ya unavyofikiri binadamu.

Malaika aliwapasha habari wachungaji wa makondeni, kwamba amezaliwa MWOKOZI ndiye KRISTO BWANA. Yesu ndiye Mwokozi wa ulimwengu, je siku ya leo Kristo bado ni mwokozi wako?, je umemruhusu maishani mwako akukomboe/akuokoe?.
 
Wafilipi 2:9-11, Jina la YESU ni la dhamani sana, kila goti litapigwa mbele zake wala hakuna jina jingine zaidi ya jina la YESU. ukiita jina "Godfrey!" yule mtu anayeitwa Godfrey atakuja kwako kwasababu Godfrey sio jina bali ni mtu na usipomuita hatakuja, sasa unapoita jina YESU atakuja Yesu Kristo kiukweli na uweza wake na Yeye ni Mungu kwahiyo Mungu atakuja. Ukiliita jina la YESU atakuja kwako BINAFSI KWENYE MAISHA YAKO lakini usipomuita hatakuja.

Je Krisimasi ya leo unaisherehekeaje? Je unafurahi tu kula kuku na pilau? Usiwaze tu kula bali leo ni siku ya habari njema, toka waambie watu ambao hawajampokea Yesu, kwamba tunakumbuka kuzaliwa kwa Yesu, Yesu Mkombozi wa maisha yetu anayeweza kukomboa maisha ya kila mtu.

No comments:

Post a Comment