''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, January 15, 2017

MUNGU HUSIKIA NA MUNGU HUKUMBUKA

Mhubiri: Mch. Amosi Hulilo kutoka Mwanza
Maandiko: Kutoka 2:23-24,Kutoka 3: 7-10,Isaya 55:8-11,Mwanzo 8:1-4,1Samweli 1:1-3,
1Samweli 1:19-20,Mwanzo 30:22-24

Mungu Husikia na Mungu Hukumbuka. Hata miaka mingi imepita na siku nyingi zimepita Mungu unayemwabudu anasikia na anakumbuka. Unapoona siku nyingi miaka imepita usizani kuwa Mungu hajakusikia au amekusahau, bali tambua kwamba unavyomuomba anakusikia na anakukumbuka na atafanya kwa wakati wake.

Mungu hata kama amekuahidia jambo kama hautasema nae kwa kuomba na kulia mbele zake hutaweza kupata hilo jambo, na sio kwamba anakuwa amekusahau bali anataka kuona bidii yako na kwa kiasi unamaanisha kuhitaji hicho kitu, na usipoomba na Yeye anakaa kimya. Kutoka 2:23,3:7-10, Wana wa Israeli walipokuwa utumwani waliteseka  miaka mingi ikapita kwasababu hawakumlilia Mungu kwa kumaanisha, lakini baada ya miaka Zaidi ya 400 kupita ndipo walipoanza kumlilia Bwana kwa kumaanisha, ndipo alipoitimiza ahadi aliowaahidi, Mungu akawaokoa na mkono wa Farao kupitia Mussa. 
Mungu akakumbuka na akasema nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri na hii ilikuwa ni baada ya wana wa Israeli kulia mbele za Mungu.

Mungu akiamua kukukumbuka hakukumbuki peke yako, Mwanzo 8:1-4. Inawezekana kuna mambo mengi ambayo hayajitimia katika maisha yako lakini usikate tamaa, endelea kumuomba Mungu kwa bidii maana YEYE husikia na hukumbuka. Mungu hakukumbuki upande mmoja bali hukukumbuka pande zote, hatakumbuka ofisini kwako tu au masomo yako tu bali na familia yako na afya yako.
 
Unapofanikiwa mambo yako usifikiri una akili kuliko wengine bali ni kwasababu wakati wa Mungu kwako umefika! ndio maana ameachilia kufanikiwa kwako na wakati wa Mungu ukifika katika maisha yako hakuna anayeweza kuzuia mipango ya Mungu. Simama na Mungu na Mungu atashughulika na wewe.

No comments:

Post a Comment