''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 29, 2018

UTUKUFU WA KRISTO

Mhubiri: Mch. Mussa Elias
Maandiko: Marko 9:1-13

Yesu alienda na Petro, Yakobo na Yohana mlimani, mara gafla Yesu akabadilika sura yake, na mara Musa na Elia wakaonekana. Uwepo wa Kristo ukawa mwingi, mpaka Petro akaanza kuongea maneno ambayo hata yeye kwa wakati ule hakuelewa kwanini anaongea hayo. Uwepo wa Mungu unaposhuka unakuwa na nguvu sana mpaka kwa akili za kibinadamu huwezijua cha kufanya. Hawa walifurahia sana sana uwepo wa Mungu mpaka akajisahau mwenyewe akasema watengeneza  vitatu tatu akajisahau mwenyewe. Unajua uwepo wa Mungu ukishuka kisawasawa huwa inakufanya kujisahau mwenyewe na kufikiria tu kuhusu Mungu.

Hili tukio la Musa na Elia kutokea na Petro na Yohana kuwepo, hapa Yesu alikuwa anatambulisha rasmini muunganisho wa Agano jipya na Agano la kale, kwahiyo wale walikuwa ni mashahidi wa agano la kale na jipya, mashahidi wa utukufu wa Mungu. Mungu akasema kabisa kuwa huyu(Yesu) ni mwanangu mpendwa, huu ni muda ambao alimtambulisha vizuri. Unajua agano la kale manabii peke yao ndio walikuwa wanafanya miujiza na kuwasiliana na Mungu kwahiyo Wayahudi walikuwa wanawaabudu manabii tu mpaka wakati huo, kwahiyo hapo Mungu alikuwa anaweka sawa kwamba hakuna wakuabudiwa mwingine zaidi ya Yesu Kristo.

Kwenye 2Petro 1:16-21 hapa ndipo Petro mwenyewe anadhibitisha kile kilichotokea mlimani maana na yeye Petro alikuwepo siku hiyo. "16 Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. 17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. 18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu. 19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu."

Utukufu wa Mungu unaposhua; Mungu huongea, magonjwa huondoka. Wakati safari ya wana wa Israel, waliongozwa na wingu mpaka wingu liondoke ndipo na wao walikuwa wanatembea, bila utukufu wa Mungu huwezi fanya kitu chochote. Utukufu wa Bwana ukikujia hutachelewa kanisani, hutaangalia muda kuwahi kumaliza ibada kwasababu inakufanya usitake kuondoka hiyo sehemu. Kwahyo tunahitaji utukufu wa Mungu katika maisha yetu, katika ndoa zetu katika familia zetu. 

Kama ambavyo samaki asivyoweza kuishi nje ya maji, ndivyo sisi ambavyo hatuwezi kuishi au kufanya vitu kwendana na mapenzi ya Mungu, bila utukufu wa Mungu. Magonjwa hayawezi kukaa kwenye utukufu wa Mungu, Unaupataje na kuutunza utukufu wa Mungu ni kwa kusoma Neno la Mungu sana na kuomba kwa bidii, vile unavyomkaribia Mungu na kuwa naye karibu ndivyo utukufu wa Mungu utakavyozidi ndani yako.

No comments:

Post a Comment