''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, August 12, 2018

FURAHA YA KUMTUMIKIA MUNGU

Mhubiri: Mzee Kiongozi, Dr. Mumghamba
Maandiko: Luka 10:17-20

Luka 10:17-20
"17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni."

Wanafunzi wa Yesu walifurahi sana kuona kwamba pepo wanawatii. Hii ni furaha ambayo waliipata baada ya kukubali kwenda kufanya kazi ya Mungu. Ukifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu kuna faida nyingi sana zitakazo ambatana na wewe, na mojawapo ni furaha. Furaha ya kweli haitoki mahali kwingine kokote bali ni kwa Yesu tu, unaweza kuwa na pesa nyingi lakini usiwe na furaha. 

Lakini usiishie kuokoka alafu ukakaa tu bali baada ya kumjua Mungu anza kufanya kazi yake kwa uaminifu. Kila mtu uliyeokoka unayo agizo maalum la kutimiliza, na agizo hilo linatoka, Marko 16:15-20 "15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. 19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo."  

Umepewa agizo la kuwahubiri kwa watu wote, anza leo kuwaambia watu habari za Yesu. na katika kazi hiyo Yesu hakutuacha hivi hivi bali alitupa nguvu zaidi; Mathayo 16:18-19 "18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

Kwahiyo mtumikie Mungu kwa kujiamini ukijua kwamba nguvu hiyo umepewa.

No comments:

Post a Comment