''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, July 22, 2018

NJAA NA KIU YA HAKI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Mathay 5:1-12
Mstari mkuu: Mathayo 5:6

Njaa na kiu ni ule msukumo wa ndani wa kutaka kitu fulani, ni uhitaji mkubwa wa kutaka kitu fulani. Mtu akiwa na njaa ya chakula, ile njaa itamfanya atafute kwa bidii atapata wapi kitu cha kula ili atulize uhitaji ule. Vivyo hivyo tunatakiwa tuwe na njaa na kiu ya Neno la Mungu. Je ni mara ngapi una kiu ya kusoma Neno?, kiu ya kutafakari Neno la Mungu? 

Hizi ni siku za mwisho wengi wanapanga mambo yao tu na kuyaweka kipaombele na kusahau muda na Mungu wako. Je wewe binafsi ni mara ngapi unapanga muda maalum wa kusoma Neno? na muda wa kuomba?, wengi mnaomba dakika mbili tu lakini kwenye mambo mengine uko tayari kutumia muda mwingi huko, lakini muda wako kumpa Mungu aliyekuumba unaona shida. 

Watu wako tayari kuwa makini kuangalia mpira dakika 90 lakini kusikiliza Neno kwa dakika 60 tu wanaona ni shida kwanini kwasababu hawana kiu ya kusikiliza Neno la Mungu na huku ndiko kufa kiroho. Hata kama huombi nyumbani je una kiu ya kuja maombi ya kanisani? badilika leo mpendwa, anza kuwa na kiu ya kusoma Neno la Mungu na kuomba maana bila hivyo mambo ya dunia yatakuvuta na hutaiona mbingu.

Yesu alikuwa asilimia 100 mwanadamu na asilima 100 Mungu, lakini na Yeye alikuwa na ratiba kabisa ya kufanya maombi yake binafsi, mara nyingi alikuwa anapanga mlimani anaomba usiku kucha, anatafuta muda wake mzuri na Baba yake. Sasa kama Yesu alifanya hivyo alivyokupa hapa duniani, sisi je?. Usipoomba dunia haiwezi kukuacha ni lazima tu utabebwa na mambo ya dunia, kama husomi Biblia huwezi kushida mambo ya dunia. Inakupasa kila siku kutenga muda wako na Mungu.

Je, huwa unatafakari kuhusu kurudi kwa Yesu au mwisho wako utakuwaje? Ni matamanio yangu kuwa ubadilike leo uanze kusoma Neno la Mungu hata sura 2 kwa siku. 

No comments:

Post a Comment