--------------------------------------------------
Huo ndio ujumbe wa jumapili uliofundishwa na Mch. Peter Mitimingi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Neno lilikuwa, Mathayo 13:24-25, Mchungaji alikazia katika dondoo 3 za muhimu
1. Watu wanapolala ndipo adui anapoanza kazi zake za
uharibifu. Mpanzi alipolala ndipo adui alipopata nafasi ya kupanda magugu katika shamba lake. Adui
alisubiri mpaka mpanzi alipolala ndipo akapanda mbegu mbaya, shetani anasubiri
mpaka ulale kiroho ndipo apande mawazo na roho chafu moyoni mwako. Usipokuwa makini
shetani hung’oa na kuharibu Neno la Mungu lililokuwa ndani mwako.
2. Shetani anasubiri unapolala ndio afanye kazi zake,
shetani hana uwezo wa kupora haki zako mchana wakati upo macho. kwahiyo
atakubembeleza na kukutengenezea mazingira mazuri ya wewe kulala ili apate
nafasi ya kuharibu maisha yako, 1 Wafalme3:20. Kama utakuwa hai kiroho shetani
kamwe hataweza kukuibia haki zako.
3. Kanisa la Mungu Tanzania linasinzia na kumpa nafasi
shetani ya kuliibia, watakatifu wengi sasa wamekuwa wavivu kuomba na kusoma Neno
la Mungu, wengi sasa wamekuwa wakijali kazi na biashara kuliko kumtafuta Mungu. Acha kumpa nafasi ibilisi, badilika sasa ili uiokoe Tanzania na zaidi ya yote ufike Mbinguni.
ANGALIA VIDEO YA MAHUBIRI
Wanafunzi wa Alpha sec school wakisikiliza Neno la Mungu
No comments:
Post a Comment