MAANDIKO: Wakolosai 2:6-7, Wakolosai 3:1-7
MHUBIRI: Mch. A.M.Mhini
Tuliambiwa tukae ndani ya Roho Mtakatifu tangu siku ya
kwanza tuliookoka lakini hali hii imekuwa ikipungua polepole ndani ya makanisa
yetu, Wastu wengi sasa wamekuwa hawaoni umuhimu wa kuaka ndani ya Roho
Mtakatifu na wengi wao wamempoteza kabisa kwasababu ya kuipenda dunia na mambo
yake zaidi ya kumpenda Mungu.
Inawezekana kabisa ulikuwa mzuri katika maombi, ulikuwa sio
mzito kufunga na kuomba, ulikuwa unakuja sana katika mkesha, lakini sasa
umepunguza au umeacha kabisa. Kama una hali hiyo jua kwamba kuna kitu cha
muhimu kimepungua ndani mwako nacho ni Roho Mtakatifu, Umemuacha Roho Mtakatifu.
Huna hamu tena ya kusoma Biblia/Neno la Mungu, huna hamu tena ya kuomba ni
kwasababu Roho Mtakatifu hayupo ndani mwako.
Ni kweli ulijazwa Roho Mtakatifu siku zilizopita lakini sasa
hayupo hai ndani mwako ameondoka ndani mwako ni kwasababu wewe ndie
uliyemuacha, matendo yako ndio yaliyo mfukuza ndani mwako. Umekuwa mzito kuja
kwenye ibada za katikati ya wiki, umekuwa huna mguso tena wa kutii matangazo
yanayotangazwa madhabahuni.
Mara ngapi umeambiwa uje ibada za katikati ya wiki hujaja?
Kwanini?, Rooho Mtakatifu ameondoka ndani mwako. Sahivi ukifanya dhambi roho
haikusuti tena unajisikia kawaida kabisa, Vitu visivyo vya kawaida unaviona
kawaida ni kwasababu huna Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndicho chombo muhimu
katika wokovu
No comments:
Post a Comment