Mhubiri: Mch. Michael Salaka
Maandiko: Warumi 10:13-15, Yohana 14:12, Isaya 47:13
Kanisa la sasa linaongezeka kwa namba lakini nguvu ya Mungu imepungua, watu wamepunguza maombi, watu hawako tena kuifanya kazi ya Mungu jinsi inavyopasa, yawezekana umeshajiwekea siku za ibada za kati kati ya wiki kuwa hauji na unafikiria hiyo ni haki yako au ni sawa eti kwasababu uko busy kazini, umeacha kuja kwenye mikesha unaona watu fulani ndio wanahitajika sana kuja kwenye mkesha, inawezekana hausemi wazi wazi lakini wewe kazi yako ni kulala unawaacha watoto ndio waende wewe ubaki. Kuna Mtu alizungumza kitu cha ajabu sana akasema Yoel 2:28 wazee wataota ndoto maana wazee kazi yao ni kulala pia akasema ninyi vijana kazi yenu ni kuona kwahiyo muende kanisani kwenye mkesha hiyo ni injili ya uongo.
Lakini maandiko yanatuambia hivi tunatakiwa kufikia kimo cha utimilifu wa Kristo, Yohana 14:12 "Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba." wapendwa hiyo ndio injili tuliyopewa kuihubiri, hiyo ndio injili ya Bwana Yesu. Pia wako watu wanaosema watu wanakimbilia miujiza tu wakisikia miujiza huku wanakwenda lakini hao ni sawa na mafarisayo na makuhani walivyokuwa wanasema mkitaka kuponywa msubiri siku nyingine lakini sio siku ya sabato na wakajiona kuwa wako kiroho, sasa ngoja nikwambie a standard gospel ya Bwana Yesu ni lazima uweza na Nguvu za Mungu uonekane na Yeye aonekane ajidhihirishe katika watu ajiinulie utukufu. Pia injili tunayotakiwa kuhihubiri ni lazima ifikie kiwango cha kitabu cha matendo ya mitume lakini siku za leo kuna vihoja vingi vya ajabu. Ninakushauri ni kwamba simama katika Neno hilo ndilo litakalo kuokoa.
No comments:
Post a Comment