''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, October 26, 2014

NENO LA UMISHENI - Na.MCHUNGAJI MLOKOZI WA UBUNGO TAG

UJUMBE:JISHUGHULISHE NA NENO LA MUNGU
NENO KUU:1Wakorintho 3:1-9

1 KOR 15:48, LUKA 5:1-8, 1PET 1:23-25, 2PET 1:3-5, WARUMI 12:1, WAKOLOSAI 3:16, YOH 15:7, YOSHUA 1:8, WAGALATIA 5:19,22

TUNAJISHUGHULISHAJE NA HII MBEGU AMBAYO NI NENO LA MUNGU?

"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, NA MANENO YANGU YAKIKAA NDANI YENU, OMBENI MTAKALO LOTE NANYI MTATENDEWA".


Hili Neno aliliandika Paulo kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu kuhusiana na kanisa la Korintho, aliliandikia baada ya kupata habari kuwa yametokea mambo ya kuligawa na kulichafua kanisa, walikuwa wanaendelea na tabia zao ambazo sio nzuri japokuwa walikuwa wameokoka, vipawa vinafanya kazi lakini mienendo yao ilikuwa haionyeshi badiliko la kweli mbele za Mungu na mbele za wanadamu, kwahiyo kanisa likaanza kuingia kwenye matatizo. Mji wa Korintho ulikuwa ni mji uliochafuka sana, na Mungu aliwaokowa watu wale ili wawe kielelezo katika mji ule lakini hawakuleta tazamio lile lililokusudiwa.

Apolo na Paulo wote walikuwa ni watumishi wa Mungu tu jukumu walilotenda ni kupanda Neno la Mungu kwenye mioyo ya wakorintho kwahiyo wote walifanya kazi sawa kwahiyo haijalishi nani aliyepanda bali kusudi la muhimu ni kupanda Neno la Mungu, lakini wakorintho wakataka kugawana wa Paulo na wa Apolo, chanzo cha shida hii ni lile pando la Neno halikuzalisha kile kilichotarajiwa, bali kilichoonekana korintho ni matokeo ya kitu ambacho Paulo hakukipanda na wala Apolo hakukipanda. Tatizo walilokuwa nalo sio la Paulo au la Apolo bali ni la wao wenyewe vile walivyokuwa. Kila mtu anawajibika na atatoa taarifa zake mwenyewe. Hatuendi Mbinguni kama kudandia daladala linaloenda mbinguni, hapana! bali tunaenda Mbinguni kwa vile jinsi ulivyoishi hapa duniani.

Neno la Mungu limekusudiwa lipandwe kwako na lizalishe matunda lililokusudiwa, lakini Neno la Mungu halitatoa matunda yaliyokusudiwa kama hutajishughulisha na Neno vile ipasavyo, na usipo jishughulisha nalo hulipi nafasi ya kuzaa yale matunda yaliyo kusudiwa, kuleta tabia iliyokusudiwa, kuleta upendo uliokusudiwa ndani ya moyo wako. Usipolipa nafasi Neno la Mungu ndani ya maisha yako utaendelea kuwa mtu wa kawaida kama wale wasio okoka kwasababu huliachii Neno nafasi ya kukubadilisha na kuleta matokeo yale yaliokusudiwa ya kuwa kiumbe kipya katika Bwana wetu Yesu Kristo.

Mungu anatarajia tuishi maisha ya rohoni, kwa kuwa Mungu ni roho, ili tupate nguvu ya kuzaa matunda mengi na mageuzi kupitia Neno la MUNGU. Neno la Mungu lina nguvu sana, na roho hutenda kwenye neno kama YESU alivyoo jaa neno la MUNGU alipokuwa duniani. Unavyoitwa mkristo Mungu anategemea uwe na tabia za Kristo katika maisha yako.


No comments:

Post a Comment